ad

ad

Rais Kikwete aitaka Tanesco kuwasha mitambo yote ili kupata umeme wakutosha



Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameridhishwa na ujenzi wa uwekezaji wa mradi wa kituo cha kufua umeme wa mitambo ya gesi asilia cha Kinyerezi One uliogharimu shilingi bilioni 400 na kulitaka shirika la umeme nchini kuhakikisha kazi ya kukamilisha kuwasha mitambo mitatu iliyobakia inakamilika haraka ili kuondoa malalamiko ya kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika nchini.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea mitambo hiyo na chumba maalum cha wataalamu wanaoongoza mitambo hiyo na kuzindua mradiwa mtambo wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi One wenye uwezo wa megawati150 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia miamoja.
 
Aidha Dk Kikwete amelitaka shirika hilo kutumia vyanzo vya umeme wa gesi asilia kama fursa ya kufanya biashara ndani na nje ya nchi.
 
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini Tanesco injinia Felsheslim pamoja na kuelezea mtambo huo kuwa ni wa kisasa una uwezo wa kutumia gesi asilia ama mafuta mepesi ya kuendeshea ndege amesema tayari umeme wa gesi umekwishaingia kwenye gridi ya taifa  kupitia nyaya zenye msongo wa kilovati 220 na katika ubora wake kamwe hairuhusu kushindwa kuzalisha umeme.
 
Awali Tanesco iliwasha mitambo yake ya umeme wa gesi Septemba 17 katika kituo chake cha Ubungo jijini Dar es Salaam na tayari megawati 200 hadi sasa zimekwishaingia ambapo pia shirika la umeme Tanesco likamzawadia rais Kikwete picha maalum yenye miradi mbalimbali ya umeme ambayo ameitekeleza wakati wa kipindi chake cha uongozi kwa miaka kumi ikiwa ni suluhisho la upatikanaji wa umeme wa uhakika hapa nchini.
Powered by Blogger.