Upepo umegeuka...Mtaji wa kura ni mikoa 9, Ukawa, CCM hakuna kulala
Na Mwandishi Wetu ZIKIWA zimebaki siku 16 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, upepo wa kisiasa unaonekana kugeuka kati ya wagombea wawili wa kiti cha urais, Dk. John Magufuli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Katika mwenendo huo wa kampeni, Uwazi Mizengwe limebaini kwamba, mgombea wa CCM Dk. Magufuli ameonekana kuja kasi katika siku za mwisho kulinganisha na wakati zilipoanza kampeni hizo, huku akifanikiwa kuvunja ngome imara zinazodaiwa kuwa ni za Ukawa. Wakati kampeni hizo zilipozinduliwa Agosti 22, 2015, ilionekana dhahiri kwamba Lowassa alikuwa amemfunika Magufuli kwa wingi wa watu kwenye mikutano yake, lakini hali sasa imekuwa tofauti. Hayo yamejidhihirisha katika mikutano ya hivi karibuni ya Magufuli, hususan katika Mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro alikomalizia ziara jana, ambako alikusanya umati mkubwa wa watu huku akitamba kwamba tayari amekwishazivunja ngome za Chadema na Ukawa. “Kama wanasema tunatengeneza picha hizi za mikutano yetu ambayo inaoneshwa moja kwa moja kwenye runinga basi nendeni mkawaambie kwamba ngome zao zimevunjwa… nipeni kura niingie ikulu nitatue kero zenu,” alisema Magufuli katika mikutano yake mbalimbali Kanda ya Kaskazini ambako inaaminika kwamba ndiko iliko ngome ya Chadema. Wagombea wote wawili wameonekana kujikita katika mikoa tisa ambayo ina wapiga kura wengi wakiamini kwamba kama watafanikiwa kuwashawishi wapiga kura hao 12,119,263 (asilimia 50.96) ya watu wote waliojiandikisha, basi wanaweza kushinda. Jumla ya Watanzania 23,782,558, sawa na asilimia 99.5 ya matarajio, walijiandikisha mwaka huu kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kupitia mfumo wa mashine za kielektroniki (BVR). Takwimu za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) kuhusu wananchi waliojiandikisha katika mikoa tisa inayogombewa zinaonesha kwamba Arusha ina wapiga kura 1,000,870 (sawa na asilimia 4.21), Dar es Salaam imeandikisha watu 2,845,256 (11.97%), Mwanza ina wapiga kura 1,442,391 (6.06%) na Mbeya wapiga kura 1,373,000 waliojiandikisha sawa na asilimia 5.77. Aidha, Morogoro ina wapiga kura 1,272,140 (5.35%), Tabora ina wapiga kura 1,083,926 (4.56%), Dodoma 1,053,136 (4.43%), Kagera 1,039,268 (4.37%), na Tanga imeandikisha wapiga kura 1,009,276, sawa na asilimia 4.24. Mbali na mikoa hiyo tisa, mikoa mingine ambayo gazeti hili limefanikiwa kupata idadi ya
waliojiandikisha ni Mara yenye watu 884,985, sawa na asilimia 3.72 ya watu wote waliojiandikisha. Mikoa mingine ambayo nayo imekuwa na mvutano katika siasa za vyama vingi ni Shinyanga ulioandikisha watu 768,270 (3.23%), Kigoma 794,463 (3.34%), Lindi 569,261 (2.4%), Ruvuma 826,779 (3.48%), Mtwara 682,295 (2.87%), Iringa 526,006 (2.21%), Kilimanjaro 794,556 (3.34%) na Manyara watu 673,357, sawa na asilimia 2.83 ya wote waliojiandikisha. Kitu ambacho kimemfanya Magufuli aanze kupaa ni uwezo wake wa kujieleza kwa muda mrefu, kubadilika kulingana na mazingira ya mahali anakofanyia mikutano, kujikosoa kwa kuwashambulia watendaji wa serikali wazembe, uwezo wa kusafiri muda mrefu kwa kutumia barabara pamoja na kutumia lugha rahisi inayoeleweka kwa wananchi. Hata hivyo, Magufuli amefanya mikutano mingi zaidi ya Lowassa ambapo hadi tunakwenda
mitamboni, licha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 20,000 katika mikoa 22, wilaya 125 na vijiji 6,120, ambako amehutubia mikutano rasmi 186 na mikutano 492 isiyo rasmi kwa kusimamishwa na wananchi. Kitendo cha wapambe wa Magufuli kuendelea kuzungumzia kuzorota kwa afya ya Lowassa kinampunguzia alama mgombea huyo wa CCM kwa kuwafanya wananchi wampe ‘kura za huruma’ mgombea wa Ukawa. Lakini mambo mengine yanayoelezwa kuwa kikwazo kwa Magufuli ni vitendo vinavyofanywa na watendaji wa serikali kwa sasa kama huduma duni za afya, kukatika ovyo kwa umeme kunakoathiri uchumi na tetesi za
kuwepo kwa mivutano ya ndani. Lowassa kwa upande wake amefanya ziara katika mikoa 27 na kufanya mikutano rasmi 110. Kinachomwangusha Lowassa ni afya yake na kushindwa kujieleza kwa muda mrefu huku akiwategemea zaidi wapambe wengine, hasa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye. Wakati Lowassa anapewa dakika tatu hadi tano tu kuomba kura huku akizitumia kuomba kura bila kunadi sera, CCM wanampa Magufuli muda wa dakika 45 hadi saa 1:15 katika kampeni hizo. Inaelezwa pia kwamba, kuondoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba kwenye Ukawa ni pigo kubwa kwa wapinzani hao ingawa hawataki kusema hadharani. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaeleza kwamba, mabadiliko zaidi yanaweza kujitokeza kadiri tarehe ya uchaguzi inavyokaribia
CHANZO: UWAZI MIZENGWE

Post a Comment