SINGIDANI (A Story From My Heart) - 34

Mchungaji Massawe alianza kwa
kumwuliza Chris: “Christopher Joseph Shila, upo tayari kuoana na huyu Laura
John Ngeleja awe mke wako, ushirikiane naye katika shida na raha, hadi kifo
kiwatenganishe? Kama ndivyo, sema ndiyo Mungu anisaidie.”
Chris hakujibu kitu!
SASA ENDELEA...
Chris hakujibu kitu!
SASA ENDELEA...
HISIA kali ilimshika Chris. Ni kama
alikuwa kwenye ndoto ya kusisimua. Hakuamini kama ni yeye alikuwa mbele ya
kanisa akiwa amevaa suti kali nyeusi na shati jeupe huku shingoni akiwa amevaa
tai fupi nyekundu!
Laura alitingisha! Alivaa gauni
jeupe na shela iliyoburuzika hadi chini. Furaha ikamfanya asahau kuwa yupo
kanisani na alitakiwa kujibu swali la Mchungaji ili kukamilisha uhalali wa ndoa
yao.
Kanisa zima lilikuwa kimya. Wengine walianza kuogopa, wakahisi huenda Chris aliamua kubadilisha mawazo. Kwamba aliamua kuachana na suala la ndoa na Laura.
Haikuwa hivyo.
Kanisa zima lilikuwa kimya. Wengine walianza kuogopa, wakahisi huenda Chris aliamua kubadilisha mawazo. Kwamba aliamua kuachana na suala la ndoa na Laura.
Haikuwa hivyo.
Chris alimpenda sana Laura,
alichanganywa na tukio lililokuwa mbele yake ambalo lilikuwa kama sinema ya
kusisimua.
“Christopher...” Mchungaji akaita.
“Naam!”
“Christopher...” Mchungaji akaita.
“Naam!”
“Hujaona sehemu ya kusoma kijana
wangu?” akauliza Mchungaji.
“Nimeona.”
“Nimeona.”
“Sawa, nami nitakuuliza tena:
“Christopher Joseph Shila, upo tayari kuoana na huyu Laura John Ngeleja awe mke
wako, ushirikiane naye katika shida na raha, hadi kifo kiwatenganishe? Kama
ndivyo, sema ndiyo Mungu anisaidie.”
“Ndiyo Mungu anisaidie,” akajibu
Chris.
Ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe na nderemo. Matarumbeta nayo hayakuwa nyuma, yalisikika yakipulizwa na hivyo kuamsha shangwe ukumbini humo.
Ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe na nderemo. Matarumbeta nayo hayakuwa nyuma, yalisikika yakipulizwa na hivyo kuamsha shangwe ukumbini humo.
Mchungaji akamgeukia Laura kisha
akamwuliza: “Laura John Ngeleja, upo tayari kuoana na huyu Christopher Joseph
Shila awe mume wako, ushirikiane naye katika shida na raha, hadi kifo
kiwatenganishe? Kama ndivyo, sema ndiyo Mungu anisaidie.”
“Ndiyo Mungu anisaidie,” akajibu Laura.
“Ndiyo Mungu anisaidie,” akajibu Laura.
Kelele zikazidi kuwa kubwa, kanisa
zima lilishangilia. Ilikuwa furaha kwa wote. Zoezi lililofuata baada ya hapo
ilikuwa ni kuvalishana pete.
Ndoa ikawa imefungwa!
Chris na Laura wakawa mume na mke rasmi.
***
Sherehe ilikuwa katika Ukumbi wa Mlimani City. Hiyo ilikuwa ni baada ya maharusi na ndugu wengine kuzunguka sehemu mbalimbali za jiji na kupiga picha.

Waandishi wa habari walikuwa mstari
wa mbele kuhakikisha wanapata picha nzuri za kupamba magazeti yao. Chris kuoa
ilikuwa habari kubwa sana kwa magazeti Pendwa Bongo.
Waandishi na wapigapicha maarufu,
Issa Mnally, Richard Bukos na Shakoor Jongo walikuwa wanashindana kutafuta
picha bora zaidi ambayo ingependekezwa kutokea kwenye ukurasa wa mbele wa
Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu.
Achana na hao, wapigapicha wa
magazeti mengine ya kila siku na michezo walipigana vikumbo kupata picha nzuri.
Msanii wa Bongo Muvi kuoa halikuwa jambo dogo!
Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City,
wasanii walikuwa wengi sana. Walialikwa watu maalum tu. Viongozi kadhaa wa
kiserikali walikuwemo, wabunge, mawaziri, wakuu wa wilaya na madaktari.
Ilikuwa sherehe yenye heshima kubwa sana. Chris alijisikia mwanaume kamili kati ya wanaume. Wapambe wao walikuwa ni wasanii wa filamu, Jaybee na mkewe Vanessa.
Ilikuwa sherehe yenye heshima kubwa sana. Chris alijisikia mwanaume kamili kati ya wanaume. Wapambe wao walikuwa ni wasanii wa filamu, Jaybee na mkewe Vanessa.
MC wa shughuli hiyo alikuwa ni
Chika, ambaye siku zote amekuwa akiongoza hafla mbalimbali za wasanii na watu
wengine. Kwa Chris ilikuwa siku mpya ya kipekee ambayo ilikamilisha haja ya
moyo wake.
Wenye kunywa walikunywa sana. Chakula kililiwa hadi kikabaki. Fungakazi ilikuwa zawadi, watu walitoa zawadi nyingi sana, achilia mbali wazazi wa pande zote ambao waliwazidi wote.
Wenye kunywa walikunywa sana. Chakula kililiwa hadi kikabaki. Fungakazi ilikuwa zawadi, watu walitoa zawadi nyingi sana, achilia mbali wazazi wa pande zote ambao waliwazidi wote.
Alianza mzee Shila: “Umefanya kitu
kikubwa sana mwanangu. Leo umenifanya nijisikie baba yako kamili. Nakupenda
sana mwanangu. Kuhusu namna ya kuishi na mwenzako tumeshazungumza mengi, najua
umeyashika.
“Kuna kitu ambacho nataka kukisema
mbele ya watu wote hapa. Kwa tendo hili, nasema kwamba nimebadili fikra zangu.
Nilichukia sana mwanangu kutokuoa mapema, lakini sikutaka kusikia anaoa mjini.
“Akilini mwangu niliamini wasanii wote ni wahuni, wana tabia mbaya na ni watu wasiofaa kwenye jamii. Kumbe nilikuwa nawaza tofauti. Nikadhani mke sahihi lazima atokee kijijini, kumbe siyo kweli.
“Akilini mwangu niliamini wasanii wote ni wahuni, wana tabia mbaya na ni watu wasiofaa kwenye jamii. Kumbe nilikuwa nawaza tofauti. Nikadhani mke sahihi lazima atokee kijijini, kumbe siyo kweli.
“Leo hii mwanangu amepata mke mwema,
sahihi na mzuri ambaye atamsaidia kama vitabu vinavyosema. Ninawabariki wanangu,
mkaishi kwa amani na upendo. Kuanzia sasa, sina kinyongo na kazi ya mwanangu
Chris. Pamoja na kwamba nilikulazimisha kusomea udaktari, nashukuru unaifanya
kazi hiyo vizuri.
“Unasaidia kuokoa maisha ya
Watanzania wengi kupitia taaluma yako. Wakati ukifanya yote hayo, bado pia
unafanya sanaa kama sehemu ya kipato na fani uliyoichagua na kuipenda.
Kuhusu zawadi, najua una gari la
kutembelea, lakini mimi nimekununulia jingine, litakalofanana na hadhi yako ya
ubaba, maana sasa umekuwa baba. Nimekununulia Toyota Range Rover, iko hapo nje.
Funguo zake hizi hapa,” akasema mzee Shila na kwenda kumkabidhi.
Shangwe zikaibuka upya!
Shangwe zikaibuka upya!
Chris alipokea funguo za gari, kisha
akanyanyua mkono juu na kuwaonyesha wageni ukumbini. Ghafla akagonganisha macho
na mtu ambaye hakutarajia kabisa kumuona!
Chris alishtuka sana!
Chris alishtuka sana!
Post a Comment