ad

ad

Sherehe za kusherehekea ushindi wa CCM zimefanyika ofisi ndogo za CCM zilizoko Lumumba jijini


Sherehe za kusherehekea ushindi wa kiti wa CCM zimefanyika ofisi ndogo za CCM zilizoko Lumumba jijini Dar es salaam...Wakati akitaka kumkaribisha Dk. John Magufuli Rais Kikwete amezungumza haya
Kikwete: Kuna wakati wale jamaa wa upande ule walikuwa wanachonga kuwa Magufuli hana mke nataka mumuone wote hapa.
Kikwete: Muda mfupi uliopita aliyekuwa mgombea wetu amekabidhiwa rasmi hati ya kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Tanzania
Kikwete: Wapo watu walikuwa wanachonga kuwa CCM itakufa, CCM itamfia Kikwete mikononi mwao.. Sasa wao ndio Sina hakika ya hatma yao sijui wako vipi sasa
Kikwete: Walisema ooh tukiacha baadhi ya watu CCM itameguka vipande vipande na kusambaratika, kumbe watu hawaijui CCM vizuri, sasa ndio leo waijue Vizuri CCM ndiyo hii na ina wenyewe.
Kikwete: Nawambia kuwa hawa watu waliokuja hapa kwenye mkutano hawajapewa Viroba, na duka la viroba CCM hawalijui.
Kikwete: Baada ya siku 5 nitakuwa Rais mstaafu na atakuwepo sasa ndugu John Pombe Magufuli, njoo Rais mteule uzungumze na Watanzania
Powered by Blogger.