Mgombea Ubunge Arusha Mjini, Estomih Millah (ACT) afariki dunia
Estomih Millah enzi za uhai wake.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini
kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Estomih Millah amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Ndugu Malla alipelekwa hospitali ya KCMC
jana mchana akitokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha Mjini baada
ya kulazwa kwa siku mbili baada kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.
Hali hiyo ilimtokea Oktoba 6, mara baada
ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni, Malla
alilalamikia kuhisi kizunguzungu na baadae kupelekwa hospitali ya St.
Thomas ambapo madaktari walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na
hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha
ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na
kwamba marehemu alifariki usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2015 saa saba
usiku.
Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.

Post a Comment