Mbatia atwaa Vunjo, Komu mshindi Moshi Vijijini
Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.
Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.
Kutokana na matokeo hayo, Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.
Kwa upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la Moshi Vijijini kupitia kwa mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani baada ya kada wa Chadema, Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa kusaini kuonyesha kuwa amekubali matokeo.
Kwa mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.

Post a Comment