ad

ad

Mgombea urais wa Chadema kupitia UKAWA apokelewa kwa kishindo Mwanza

Jiji la kibiashara la Mwanza limejikuta likisimamisha shughuli zake zote kupisha mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa ukiongozwa na mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa huku zaidi ya wananchi 130 wakizimia.
Swali jepesi kabisa ambalo kwa sasa kila mtanzania anaweza kulijibu, lakini kwa jiji la Mwanza sauti imepaa zaidi.
 
Kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ndani ya uwanja wa Furahisha kikatikisa afya za wakazi wa jiji la Mwanza kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu.
 
Akiwa jiji Mwanza alikuwa na kazi rahisi zaidi ya kuomba kupigiwa kura ya ushindi wa kishindo kwakuwa anania, ari na nguvu za kuhakikisha Tanzania inapata uchumi imara huku akiwataka watanzania kujiandaa vema na Oct 25 mwaka huu.
 
Wakati tume ya uchaguzi ikiwa tayari imekwisha weka bayana idadi ya vituo vya kupigia kura, umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umekwisha kubaini tatizo ndani ya tume hiyo na kutoa rai kwa watanzania.
 
Baada ya kutumia muda wake wa miaka 61 ndani ya tanu na CCM, kabla ya kukitosa chama chake cha CCM hivi karibuni, amemwagia sifa lukuki mgombea urais Edward Lowassa kwani ni kiongozi imara mwenye ndoto na Tanzania mpya, huku akitoa neno kwa watanzania.
.


Name:  2.jpg
Views: 3823
Size:  67.8 KB
Name:  4.jpg
Views: 3800
Size:  78.0 KB
Name:  1.jpg
Views: 3819
Size:  80.9 KB
Name:  3.jpg
Views: 3773
Size:  90.8 KB

Name:  5.jpg
Views: 4043
Size:  199.1 KB


Powered by Blogger.