ad

ad

Dkt Magufuli aahidi kurejesha viwanda vilivyo binafsishwa bila kuendelezwa

Chama cha mapinduzi kimesema serikali ijayo ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli kimejipanga kurejesha hadhi ya mji wa Arusha na mikoa mingine iliyokuwa na hadhi ya kuwa na viwanda kwa kuvifufua viwanda vya serikali na kurejesha vile vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji bila kuendelezwa na kutelekezwa ili viweze kuongeza ajira kwa watanzania huku mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo la Monduli akikanusha kukihama chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Komred Abdulrahaman Kinana ameyasema hayo jijini Arusha, wakati akimnadi mgombea urais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho Dkt  John Pombe Magufuli, ambaye  yuko katika mkoa wa Arusha akinadi sera za chama hicho ili kupata ridhaa ya kuwaongoaza watanzania. 
 
Akiwahutubia mamia kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake, mgombea huyo wa urasi kupitia CCM Dkt John Magufuli amesema, mara atakapo pata ridhaa ya watanzania katika ngazi ya urasi atarejesha serikalini viwanda vyote vilivyobinafsishwa bila kuendelezwa ikiwa ni pamoja na kufufua viwanda na kujenga viwanda vingine ili kuondoa tatizo la ajira kwa watanzania.
 
Akiwa mkoani Arusha mgombea uras Dkt John Magufuli alizuru kaburi la aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania enzi za Mwalimu Nyerere hayati Edward Moringe Sokoine na kusifia uadilifu na utendaji kazi uliokuwa ukifanywa na kiongozi huyo. 
 
Mgombea ubunge wa jimbo la Monduli kupitia CCM Namelock Sokoine amekanusha kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani ambapo katika mikutano iliyofanyika mtowa mbu, Monduli mjini, Longido na Arusha mjini baadhi ya waliokuwa watia nia za kugombea ubunge kupitia vyama vya Chadema na CUF wamejiunga na CCM.
Powered by Blogger.