WEMA AMTAJA MWANAUME ATAKAYEZAA NAYE
BAADA ya kupita ukimya mrefu bila kuzungumzia mapenzi, mrembo asiyepoteza ubora wake, Wema Sepetu ‘Madam’ amemtaja mwanaume anayetarajia kumzalia mtoto kuwa ni Luis Munana, raia wa Namibia.
Wema alifunguka hayo juzikati mara baada ya mwandishi wetu kutaka kujua ana mpango gani kwenye ulimwengu wa ‘malovee’ ndipo alipomwanika Luis kuwa ndiye mwanaume pekee ambaye ameshafikia hatua ya kumuamini na yuko tayari kuzaa naye kwa namna yoyote licha ya kujua ana tatizo la uzazi.
Miezi kadhaa iliyopita, Wema aliwahi kuonekana na Luis katika pati ya Instagram iliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar kisha wawili hao kudaiwa kulala pamoja katika hoteli moja jijini humo.

Post a Comment