DAVINA ACHARUKA KISA KURUDI KWA MUMEWE
FUNGUKA! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Halima
Yahya ‘Davina’ amesema anakasirishwa na ‘wambeya’ ambao kila uchwao
wamekuwa wakimuuliza atarudi lini kwa mumewe, Abdallah Shakoor ambaye
walitengana miezi kadhaa iliyopita.
“Yaani unamkuta mtu anajadili juu ya mimi kurudi kwenye ndoa yangu na wakati nilivyoondoka hakuna yoyote aliyefahamu hivyo siku ambayo nitaona inafaa kurudi kwenye ndoa yangu, nitarudi na watu watashtukia nimerudi tu mwenyewe bila shuruti ya mtu,” alisema Davina huku akiahidi kuwataja majina wambeya hao kama wataendelea kumsema.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’.
Kuonesha amechoshwa na maswali hayo yanayomfikia kupitia watu wake wa
karibu, Davina alisema hakuna mtu anayejua siri yake na siku
aliyoondoka aliondoka kwa sababu zake, hivyo siku akiamua kurejea,
atafanya hivyo.“Yaani unamkuta mtu anajadili juu ya mimi kurudi kwenye ndoa yangu na wakati nilivyoondoka hakuna yoyote aliyefahamu hivyo siku ambayo nitaona inafaa kurudi kwenye ndoa yangu, nitarudi na watu watashtukia nimerudi tu mwenyewe bila shuruti ya mtu,” alisema Davina huku akiahidi kuwataja majina wambeya hao kama wataendelea kumsema.
Post a Comment