ad

ad

Sheikh Abubakary Zubeir ndiye mufti mpya

WAJUMBE 310 wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), leo wakiwa mkoani Dodoma wamemchagua Sheikh Abubakary Zubeir kuwa Mufti wa Tanzania akiziba nafasi iliyoachwa na hayati Issa Shaaban bin Simba.
Kabla ya uchaguzi huo, Sheikh Abubakary Zubeir, alikuwa Kaimu Mufti wa Tanzania kwa kipindi cha mpito baada ya kifo cha Sheikh Mkuu, Issa Shaaban bin Simba.
Awali Sheikh Zubeir alikuwa Naibu Mufti wa Sheikh Mkuu na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa nchini.
Powered by Blogger.