NCCR - Mageuzi Waongea na vyombo vya habari, Wamjibu M/Mwenyekti na K/Mkuu wake
| Pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini NCCR Mohamed Tibanyendera akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam |
Chama hicho kimeibuka na kusema wanasikitika na viongozi hao kubadilika dakika hizi za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu kwani hatua zote za ugawaji wa majimbo hayo viongozi hao walishiriki kwenye hatua zote.
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini NCCR Mohamed Tibanyendera amejibu malalamiko hayo kwa kusema Chama hicho kimesikitika kwa kauli za viongozi hao kipindi hiki cha mwisho kwani maamuzi yote yaliyofikiwa na UKAWA yalifuata kanuni zote na kwamba hata ofisi ya Katibu mkuu huyo ndio ilikuwa inahusika katika majimbo hayo
“Sisi NCCR tunashangaa kwa kauli za katibu wetu pamoja Makamu mwenyekiti kwani Kipindi majimbo yagaiwa kwenye vyama Ofisi ya Katibu ilikuwepo na ndio ilikuwa inapanga majimbo hayo,kwani ugawaji huu wa majimbo unaaangaliwa ushindani wa kisiasa pamoja na nguvu ya eneo hilo husika,wote kwa pamoja tukakubaliana na hali hiyo sasa tunashangaa leo wanakuja kubadilika”amesema Tibanyendera
Amesema Majimbo 22 walioyopata NCCR kwa upande wa Ukawa ni mengi sana kwani ukizingatia na miaka ya nyuma
“Jamani NCCR tumekaa zaidi ya miaka 10 bila hata kuwa na mbunge hata mmoja,2010 tukanapata wabunge 4 tu wakuchagulia,sasa leo kupitia ukawa,NCCR imesimamisha wabunge 22 kupitia majimbo tofauti nchini maana yake ni zaidi mara 5 ya wabunge tuliopata sasa,huku wabunge wetu 4 waliopo wanaendelea kugombania”amesema
Tibanyendera ameongeza kuwa madai hayo wanayotoa yalitakiwa kutolewa kwenye vikao harali vya chama hicho ila kwa nujibu wa katiba ya chama hicho, kwa upande wao NCCR wanasikitika kuwa kwani
Hata hivyo Tibanyendera anadai kuwa viongozi hao walikuwepo kwenye kikao kikuu kilichofanyika tarehe 16 mwezi huu, na suala hilo wanalodai hawakulizungumia kwenye kikao hicho lakini wanashangaa leo kuibuka mbele ya vyombo vya Habari na kutua lawama kwa mwenyekiti,badala ya kutakiwa kulizungumza kwenye kikao hicho.
Aidha,Tibanyendera amewataka Wanachama vya Vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni Chadema,Cuf na NLD kupuuza madai ya viongozi hao na kuyachukulia ni watu binafsi na sio ya chama ,akidai kuwa NCCR itaendelea kuwa sehemu ya UKAWA na kitakuwa chama cha mwisho kujitoa ukawa,
Ambapo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya Octoba 25 mwaka huu na kumchagua mgombea wa Urais kupitia umoja huo Edward Lowassa pamoja na wabunge na madiwani wanaunda Ukawa.
Kuibuka kwa chama hicho kunazidi kufichua mbinu chafu zinazotumiwa na washindani wa siasa wa UKAWA ambao wanatumia kila aina ya njia ikiwemo kuwarubuni viongiza mbali mbali wa vyama vinavyounda ukawa kuibuka kwa jamii na kutoa maneno ambayo yanatazamiwa ili yaweze kuwagawa watanzania katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.
Chanzo: Fullhabari
Post a Comment