ad

ad

DK. SLAA, NENDA SALAMA BABA - USITULAGHAI ILI TUIAMINI CCM!


Na. Julius Mtatiro
Mwaka wa Mabadiliko makubwa huambatana na MAPIGO makubwa! Kwamba anatueleza mgombea wa UKAWA ni mtuhumiwa mkubwa lakini haelezi kuwa na mgombea wa CCM ni mtuhumiwa mkubwa tena wa kashfa nzito tu.
Kwamba anawashambulia wapiga kampeni wa UKAWA kina Sumaye na Masha kwa tuhuma za kipuuzi lakini hamshambulii Kinana na wapiga kampeni wa CCM ambao wana tuhuma nzito ambazo kwa nchi kama China adhabu yake ni KIFO.
Muda wote ule wa jana ulitumiwa kuwataka watanzania waachane na UKAWA na kuchagua CCM, sikuona ajenda nyingine. Hata hivyo, huyu naye atapita na enzi zake zitakwisha.
Msimamo wangu binafsi ni kutoiamini CCM kwa sababu ni chama kilichodhoofika na kimeliozesha taifa hili. Huko ndani ya CCM watu wasafi kama kina Dk. Salim Ahmed Salim hawana nafasi, ni chama ambacho wala rushwa na mafisadi ndiyo wana nafasi za kipekee.
Dr. Slaa hawezi kuwa "AUTHORITY" ya maisha yetu. Kwamba baada ya Mwinyi kushindwa akiongoza kutokea CCM, Mkapa kushindwa akiongoza kutokea CCM, Kikwete kushindwa akiongoza kutokea CCM eti Magufuli ataweza akiongoza kutokea CCM.
Ukweli wa wazi ni kuwa mtu atakayelivusha taifa hili na kulirudisha katika misingi hawezi kamwe kufanya hivyo akiwa ndani ya CCM. Kwa hiyo, kazi ya Dk. Slaa kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa mwaka huu wanalazimika kuichagua CCM na kuishi kwenye umasikini miaka mingine 10, kazi hiyo imefeli.
Watanzania hawaitaji tena EXPERIMENT kupitia CCM, zimefanyika kwa miaka 54 na kufeli, Dk. Slaa anataka tufanye experiment kupitia Magufuli na CCM katika miaka mitano na kumi ijayo, TUKATAE kwani waliomo CCM ni walewale wanaozalisha mafisadi na ufisadi, ni walewale wanaoiba mboga za watoto na mbaya zaidi wamo mulemule, kwenye chama kilekile.
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam.
juliusmtatiro@yahoo.com
Powered by Blogger.