ad

ad

Mpinzani wa Nape Jimbo la Mtama, ahamia CHADEMA

Aliyekuwa mtia nia wa ugombea ubunge Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM Ndugu Selemani Mathew Luwongo ameamua kuhamia Chadema jioni ya jana baada ya shinikizo kubwa toka kwa wananchi ambao hawajaridhishwa na mchakato wa kura za maoni ndani ya chama.

Wananchi wa Mtama wameandamana na kumtaka Ndugu Luwongo kuhamia UKAWA ili wapate kumpa ubunge maana aliyechaguliwa ndani ya CCM hakuwa chaguo lao

Wananchi wiki iliyopita waliandamana wakiwa na mabango yenye maandishi mbalimbali kama "Jimbo kwanza Vyama Baadae"


Chanzo: Jamiiforums
Powered by Blogger.