Lulu apata pigo pigo baada ya kufiwa na bibi yake mzaa mama
MSIBA!
Staa mwenye umri mdogo anayekimbiza katika filamu Bongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amepata pigo baada ya kufiwa na bibi yake mzaa mama,
Leonadina Mboneko (pichani), aliyefariki dunia juzi asubuhi katika
Hospitali ya Masana, iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Amani
mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila alisema mama yake alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu jambo lililomlazimu
kumtoa nyumbani kwake Bukoba na kumleta jijini kwa ajili ya kupata
matibabu.
“Nimehangaika
naye kwa muda mrefu ili kurejesha afya yake, lakini hali ilikuwa ngumu
hadi juzi Mwenyezi Mungu alipomchukua. Tumepata pigo kubwa sana hasa
mwanangu Lulu kwa sababu alikuwa ndiye kipenzi chake,” alisema mama
huyo.
Muigizaji
huyo aliyecheza Filamu ya Foolish Age hakuweza kupatikana kuzungumzia
msiba wa kipenzi chake huyo, lakini nyumbani kwa mama yake, mipango ya
kusafirisha mwili huo kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya mazishi ilikuwa
ikifanyika.

Post a Comment