Bei za mafuta ya Petrol imepanda kwa Tsh 92/lita sawa na ongezeko la 4.91% ukilinganisha na mwezi uliopita.Kwa mfano hapa Arusha mwezi uliopita mafuta ya petrol ilikua ni Tsh 2,282/lita kwa sasa bei Tsh 2,374/lita

Ni neema kwa watumiaji wa Diesel ambayo kwa mwezi huu imeshuka kwa Tsh 17.5/lita sawa na 0.9% pamoja na mafuta ya taa yalioshuka kwa Tsh 29.27/lita sawa na 1.55% ukilinganisha na mwezi uliopita.

Sababu kubwa ya upandaji wa gharama ya mafuta ni mrundikano wa bidhaa kutoka nje kwenye bandari ya Tanga pamoja na gharama za usafirishaji kutoka hapo Tanga kwenda sehemu mbalimbali za nchi.Soma taarifa yao ya bei hizo: Cap Prices WEF 05 Aug 2015 -Swahili.pdf