ad

ad

Breaking news: Zari ajifungua mtoto wa kike


Katika Mtandao wa Instagram Diamond Planumz amepost picha ya mama yake akiwa amebeba mtoto huku zari akiwa pembeni na kuandika “My mom’s face it’s enough to Express how i feell😍… Welcome to the world @princess_tiffah 👼”.
Hii inamaana mtoto wa Diamond Platnumz anaitwa Tiffah!!!.
MPENZI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ amejifungua mtoto wa kike leo alfajiri saa 10: 40 jijini Dar es Salaam. Mtandao huu umeongea na Meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Salam Sharaf ambaye amethibitisha taarifa hizo na kusema Zari bado yupo hospitali mpaka sasa.
-1541Kutokana na usumbufu aliodai unaweza kutokea, Salam hakuweka wazi hospitali aliyojifungulia Zari. “Ni kweli Zari kajifungua mtoto wa kike majira ya saa 10 alfajiri leo, lakini kutokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sasa siwatajii hospitali aliyojifungulia mpaka hapo baadaye” Alisema Salam. Mtandao huu unatoa pongezi wa Diamond pamoja na Zari kwa kupata mtoto wa kike.Diamond-and-Zarina-Hassan
Powered by Blogger.