ad

ad

AZIZA WA FACEBOOK - 5


ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
MIMI: Umepatia. Ila unavyoona kila mtu mwenye fedha huwa na furaha?
AZIZA: Inawezekana.
SASA ENDELEA:
MIMI: Umekosea. Umekwi-shawahi kuwasikia wale matajiri wanaojiua?
AZIZA: Yeah!
MMI: Sasa wamekosa nini wale katika maisha yao? Wana fedha, wanaweza kununua kila kitu, wana magari, wanaweza kwenda sehemu yoyote ile. Ila swali linakuja kwa sababu gani wanajiua?
AZIZA: Mmmh! Sijui.
MIMI: Hahaha! Jibu rahisi sana. Walikosa furaha, amani, wakakosa mapenzi na mambo mengine. Unapokuwa na fedha, utanunua gari ila kumbuka hautoweza kununua furaha, unapokuwa na fedha utaweza kumnunua msichana mtaani lakini ukashindwa kununua mapenzi. Umenipata hapo?
AZIZA: Kidogoooo.
MIMI: Yeah! Kila mtu hunipata kidogo, ila tukiendelea kuchati, utanipata sana tu. Utaniruhusu niwe nachati nawe kwa ajili ya kukuambia mengi usiyoyajua?
AZIZA: Yeah! Ila huwa siwi hewani muda wote.
MIMI: Hilo si tatizo. Unachotakiwa ni kunishtua kila unapokuwa hewani. Utakwenda kufahamu mengi ambayo haujayajua. Kwani unaishi wapi?
AZIZA: Nipo Masaki Dar es Salaam.
MIMI: Ndio maana.
AZIZA: Kwa nini?
MIMI: Usijali. Mtaa unaokaa ndio nitakaoanza nao siku tukianza kuchati. Kwa sasa nahitaji kusoma, naomba uniruhusu niondoke.
AZIZA: Ila pleeeaseeee naomba uniambie.
MIMI: Sijakataa. Nitakwambia tu wala usijali. Wewe ni rafiki yangu, pamoja kuwa na kila kitu, yakupasa kupata vitu vingine ambavyo haupaswi kuvinunua. Nitakwambia namna ya kuvipata na inawezekana hata marafiki zako wakakushangaa.
AZIZA: Mmmh!
MIMI: Usigune. Huo ndio ukweli. Usiku mwema Aziza.
AZIZA: Nawe pia.
Kuna nini tena? Nilichokifanya ni kutoka hewani mpaka saa sita ndio nikaingia tena, Aziza hakuwepo, nikamtafuta Eduado, nikamuona, hata kabla sijamtumia meseji, akaniwahi.
EDUADO: Vipi Sharukh Khan. Imekuwaje au bado?
MIMI: Kwisha habari yake. Anacheza na mwanasaikolojia nini.
EDUADO: Imekuwaje tena?
MIMI: Wewe usijali. Cha msingi andaa zawadi yangu.
EDUADO: Umeanza kufanikisha?
MIMI: Ndio maana yake. Unajua ukimjua mpinzani inakuwa rahisi sana.
EDUADO: Dah! Wewe noma kaka. Yaani hii kazi nimewapa watu saba, naona wengine wanambwela tu, wananiambia kila wakimtumia meseji dogo hajibu.
MIMI: Hahahaha! Hata mimi ilikuwa hivyo hivyo. Nilivyoona anashindwa kujibu, nikatumia plan B. Hapo ndipo nilipompoteza na kuchati nae sana.
EDUADO: Kwa hiyo ulichati nae?
MIMI: Yeah! Tena mimi ndiye nimemkatisha. Chezea mimi wewe.
EDUADO: Hahahah! Ebwana wewe nomaaaaa....sasa hata kukutambulisha kwa mrembo wangu mwingine naogopa.
MIMI: Wewe si ulinipa kazi kaka? Hakuna tatizo. Kazi inafanyika taratibu.
EDUADO: Duh! Kaka nashukuru sana kwa kunisikiliza. Natumaini mtoto ataeleweka tu.
MIMI: Amekwishaeleweka. Dogo amekwishaeleweka.
EDUADO: Hahahah! Basi poa sana, nimefurahi sana.
MIMI: Usijali kaka...hug.
EDUADO: Poa.
Kila kitu kikaonekana kuwa juu ya mstari, meseji moja ambayo alikuwa amenitumia ikaonekana kubadilisha kila kitu. Ile meseji ndio ambayo nilikuwa nikiitaka kuiona na kweli aliituma. Chatting zikawa zimeanza, kwa Aziza, nilihitajika kuwa makini sana kupita kawaida kwani kwa kufanya vile nilikuwa na uhakika wa kumchukua ili kumuonyeshea Eduado kwamba nilikuwa Sharukh Khan.
                    ***
Sikutaka kuleta shobo tena kwani tayari nilimuona kuku kuwa wangu kwa hiyo sikutakiwa kumshikia manati kwa kuamini kwamba jioni ikifika mwenyewe atarudi bandani. Nilipoingia hewani siku iliyofuatia, msichana Aziza alikuwepo, kajaa tele ila mtu mzima nikaamua kuchuna. Katika hili ngoja nikwambie kitu kimoja rafiki yangu hasa mwanaume kama mimi.
Unapoona kwamba kuna msichana fulani unampigia sana misele facebook, hautakiwi kila wakati umuanze wewe tu, sometimes unamchunia uone je ataweza kukutumia meseji au la. Ukiona kwamba kakutumia, basi jua kwamba anautambua mchango wako na hata kwenye ile mishemishe yako anaonekana kuifurahia. Ila ukiona nae anakaa kimya, mtu mzima poteza kwani si unajua warembo wapo wengi! Inawezekana haujapangiwa kuwa na huyo.
Nilipomuona Aziza hewani, nikamchunia kana kwamba sijamuona huku nikiamini kwamba yeye ndiye alipaswa kunitumia meseji. Ila katika kipindi hiki hasa siku ya leo, meseji zilikuwa zikiingia nyingi nyingi hasa kutoka kwa marafiki zangu wengine, bahati nzuri nilikuwa natumia kompyuta hivyo ilikuwa rahisi kuwajibu.
IBRA: Mambo vipi kaka!
MIMI: Poa. Ni aje mkuu?
IBRA: Kama kawa. Upo wapi?
MIMI: Nipo gheto aiseee nimesizi tu si unajua kijimvua nje kinazingua.
IBRA: Yeah! Hilo kweli kaka. Hivi unamuona mtu wangu hapo hewani?
Powered by Blogger.