Yanga yampa Olunga milioni 87
Nicodemus Jonas,
Dar es Salaam
YANGA imepania dili la kumnasa straika anayetikisa hivi sasa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, Michael Olunga wa Gor Mahia ya Kenya na ipo tayari kutoa dola 40,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 87.2 zinazotakiwa na klabu yake ili kuinasa saini yake.
Gor Mahia imeiambia Yanga kuwa Olunga na kiungo Khalid Aucho wanapatikana kwa dau la dola 40,000 kila mmoja na matajiri hao wa Jangwani wamesema wapo tayari kutoa fungu hilo ili kuwanasa nyota wote hao wawili ambao pia wanawindwa na Simba.
Simba iliweka bayana nia ya kuwataka nyota hao, lakini Yanga wameamua kuingia sokoni baada ya kugundua kuwa bado kikosi chao hakijatengemaa na upungufu umejionyesha kwenye michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar.
Ni kama Simba wameanza kukata tamaa kwa kuwawania wachezaji hao akiwemo kipa wao, Boniphace Oluoch kutokana na Wakenya hao kuhitaji kitita hicho kikubwa cha fedha.

Hata hivyo, kikwazo kikubwa kwa fowadi, Olunga ni suala la elimu, kwani bado ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Nairobi, akichukua Shahada ya Uhandisi mwaka wa tatu. Bado mwaka mzima amalize.
Yanga baada ya kusikia hivyo, wamechekelea na kutamba kuwa wanaweza kumudu masharti yote kuanzia suala la hela hadi kutegua kikwazo cha shule kwa Olunga.

Inasemekana Yanga wameanza mazungumzo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuweza kumfanyia uhamisho kutoka Nairobi ili akisajiliwa aendelee na masomo yake.
Taarifa zaidi zinafafanua kuwa mipango ya shule inasukwa na katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha kwa kutumia mgongo wa uhadhiri wake pale UDSM ili kufanikisha mpango huo.

“Ujue kikwazo kikubwa ni kwamba Olunga ni mwanafunzi lakini kwetu ni kitu kidogo sana, tayari katibu amewasiliana na uongozi wa chuo pale UDSM kama inawezekana kwa kumhamisha na hilo limekubalika. Suala la hela kwetu siyo ishu, zipo na tutawalipa,” alisema mtoa habari wetu.
Alitoboa siri kubwa suala la Azam na Simba kutaka kuwafanyia umafia wa kumnasa juu kwa juu Donald Ngoma wakati Yanga wakiwa kwenye mazungumzo naye, limewakasirisha Yanga na kuamua kuwaonyesha kuwa wanaweza kufanya lolote kwenye usajili.
“Tuna ushahidi jinsi Simba walivyotaka kumsajili Ngoma baada ya kujua tunamhitaji, lakini tunashukuru uongozi wa FC Platinum ulimsihi kutosikiliza timu nyingine kutokana na heshima ya Yanga kwenye soka la Tanzania. Lakini pia usisahau kwamba Deus Kaseke na Malim Busungu, Simba waliwafuata lakini tukawazidi kete na tunaamini hawatuwezi kwenye vita hii,” alitamba mmoja wa mabosi wa ngazi za juu klabuni hapo.
Alipotafutwa katibu Dk Jonas Tiboroha alikataa kuweka bayana mikakati hiyo kwa kusema kwa kifupi: “Mikakati ya kuboresha kikosi ipo, lakini siwezi kukwambia ni nani atasajiliwa, ingawa ni wachezaji wa kimataifa, maana bado hatujafunga usajili. Tusubiri lolote linaweza kutokea.”
Olunga mpaka sasa ana mabao matatu kwenye michuano hiyo huku kwenye Ligi Kuu Kenya akiwa anaongoza kwa kufunga mabao 12. Mbali na hao, Yanga pia inamtaka kiungo Yannik Mukunzi wa APR.

Post a Comment