Watu wanne wafariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi Kagera.
Watu wanne wafariki dunia hapohapo nawengine kujeruhiwa mara baada
ya basi la sabuni expres linalofanya safarizake kutoka wilayani karagwe
kwenda mwanza jijini kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya
landcrusezer iliyokuwa ikiwasafirisha mapadri kutoka bukoba kuelekea
karagwe katika eneo la bugorola wilayan misenyi.
Ajali hiyo imetokea majira sambili asubuhi katika eneo la Bugorola
wilayani Misenyi ambapo baadhi mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali
hiyo imetokea wakati Dereva wa gari ndogo aina ya landcruser alipokuwa
akijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake na kisha kukutana uso kwa
uso na basi la Sabuni Express lililokuwa na biria wapatao arobani na
tano na kusabisha vifo vya watu wanne ambao ni mapadri wawili,Sister
mmoja na mseminalisti mmoja wote walikuwa wakisafiri na gari hiyo
kuelekea karagwe.
Wakizungumza na ITV baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi
hilo wamsema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kawaida kutokana
ukungu ulikuwa kuwa umetenda barabarani.
Kwa upande wake katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera
Kiiza Kilwanila amesema wamepokea maiti nne pamoja na majeruhi kadhaa
ambao sasa halizao zinaendelea vizuri.
ITV imefika katika kituo chapolisi mkoani Kagera kwaajili
kuthibitisha tukio hilo kwa kamanda wajeshi ambapo sikuweza kumkuta na
kujaribu kumtafuta kwa njia ya simu hakuweza kupatikana.

Post a Comment