Uzuri na umbo siyo fimbo ya kumpigia mume wako!
Siku
zote nimeweka mdomoni neno linalosema kuwa mwanaume ni kifaa adimu kwa
sababu watu wanamaliza waganga, wanafanya matambiko ili wapate waume.
Cha ajabu kuna wanawake ambao Mwenyezi Mungu amewapa wanaume lakini
hawajitumi, wapo wapo tu!
Mfano,
unakuta mume anafua mwenyewe, mume njaa inamuuma mke yupo anaangalia TV
au kaenda kuzurura. Mume anavaa nguo chafu kisa mke hajali suala la
kufua. Jamani mume kwa mke ni kama mtoto, anatakiwa ale kwa wakati, avae
nguo safi.
Kuna baadhi ya wanawake wanadhani uzuri walionao na sifa zote walizojaaliwa kuwa nazo ni fimbo ya kumpigia mume.
Kumbuka
kuwa kuna wanawake wazuri sana kiasi kwamba ukiwaangalia wewe mwenyewe
unawakubali lakini wanajituma ipasavyo kwa waume zao. Sasa wewe ni nani
mpaka ubweteke hivyo?
Hebu
jitahidi kumjali mumeo, isipite siku hujamjulia hali, kama yuko mbali
na wewe mtumie hata ujumbe wa kumwambia kuwa umemkumbuka. Muulize
amekula nini, mkumbushe kuwa muda wa kula umefika na sms nyingine za
kuonesha kuwa umemkumbuka.
Utakuta
mwanamke kutwa nzima anazurura, mara yuko Kariakoo anatafuta madera,
mara kaenda kwa shosti wake Magomeni, akirudi nyumbani kachokaaa.
Mume
sasa anataka huduma unashangaa mke anadai kachoka, akifuatilia
kachoshwa na kipi, eti sababu ya kuzurura kutwa nzima, huko ni
kujiaibisha.
Mke
kama ni mama wa nyumbani au umewahi kurudi kazini au uko ‘off’, tulia
nyumbani ukimsubiri mumeo. Fanya usafi wa hapa na pale, kiandae chumba
chako kwa kutandika kitanda, pulizia manukato, udi mzuri, asmini na
kilua.
Mumeo
akirudi akukute umeshajiandaa kimawazo kumpokea. Siyo anarudi anakuta
nyumba iko vululuvululu, wewe mwenyewe unanuka jasho, utaachika kama
siyo kutafutiwa mke mwenza shoga.
Lakini
pia siyo mbaya ukatenga muda wa kumkata kucha mumeo, kumsafisha masikio
kwani mbali na kwamba kufanya hivyo ni kumfanya awe msafi, pia
kunaamsha hisia.
Mwisho nakukumbusha mwanamke mwenzangu kwamba fanya yote lakini tendo la ndoa ni haki ya mumeo na ni mhimili wa ndoa.
Kilichokufanya
ukaaicha familia yako na kwenda kwa mume siyo kula wala kufuata mali,
umefuata haki hii. Kwa maana hiyo basi, isitokee hata siku moja
ukamwambia mumeo; ‘nimechoka’ wakati yeye anahitaji.
Hii
kusema mara unaumwa, mara umechoka, mara hujisikii ni kosa kubwa na
wengi wamejikuta wakitafutiwa michepuko kwa kutokuwa makini katika
kuwatimizia waume zao.
Kumbuka
kwamba, licha ya uzuri wako na kujaaliwa kuwa na umbo zuri, usilete
maringo kwa mumeo. Uzuri wako hauwezi kuishika ndoa, wajibika kama mke
ili umfanye mumeo aamini amepata mke kwa maana halisi ya mke na siyo
toi, upo hapo shoga?
Post a Comment