Ray c awapiga mizinga wanaume wanaomchumbia
MAKUBWA! Mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C,’ amedaiwa kuwageuza mtaji wanaume wanaojitokeza kumchumbia kwa kuwapiga mizinga ili ajipatie ‘chochote’ (fedha), Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanaume aliyejitambulisha kwa jina la Aboubakar ambaye alifunga safari mpaka kwa Ray C kwa lengo la kutaka kumuoa wiki chache baada ya mwanadada huyo kutangaza kutafuta mume mwenye vigezo alivyovitaka, baada ya kuchati na kumueleza kuwa anataka kumuoa, alishangaa kuona mwanadada huyo anampiga mzinga.
Kijana Abubakar Ally ‘Babuu’.
Aboubakar alisema Ray C alimuomba amtumie shilingi laki moja kwa njia ya simu ambapo jamaa huyo alikataa na kutaka wakutane kwanza ndiyo wapeane kiasi hicho cha fedha. Msanii huyo alimtaka jamaa wakutane Mbezi-Garden lakini amtumie kwanza pesa hizo.
Akizidi kumwaga ubuyu, Aboubakar alisema alianza kumuona Ray C kama mtu wa mizinga kwa kung’ang’ania atumiwe pesa hiyo wakati hawajakutana na kuongeza kuwa alimpigia simu ili kupata uhakika zaidi kama kweli akimtumia pesa hiyo watakutana kwenye hoteli hiyo, lakini alimhakikisha kuwa endapo atamtumia watakutana.
“Unajua nini, ningeweza kumtumia kama tungekutana ana kwa ana lakini ndiyo kwanza nimewasiliana naye ananipiga kirungu kikubwa hivyo je, nikiwa naye si nitakuwa natoa mamilioni, kama ndiyo hivyo amenishinda,” alisema Aboubakar.
...Kama hiyo haitoshi, mwanaume mwingine kutoka Mwanza aliyeongea na mwandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, alidai kuwa Ray C alimwambia amtumie shilingi elfu 40 kwa ajili ya mafuta kwenye gari lake kabla hata hajakutana naye jambo lililomfanya aachane naye.
“Aliniambia nimtumie shilingi elfu 40, sasa nikaona mtu mwenyewe ndiyo kwanza ninaongea naye, anaonekana anapenda hela sana huyu mdada na mimi nimekata tamaa,” alisema mwanaume huyo.
Mwandishi wetu alimtafuta Ray C na kumsomea mashtaka yake ambapo alisema wanaume wengi wamekuwa wakimsumbua baada ya kutangaza kutaka mume na kudai kuwa wanaume hao ni washamba hivyo ameamua awaombe hela ili wasimpigie tena.
“Wapuuzi sana hao, sasa kuwakatiza nawaambia tuma milioni baada ya hapo hawanisumbui tena,” alisema Ray C na alipoulizwa kama haoni anajikosesha bahati ya mume mwema kwa kuwaomba hela, alisema wanaume wengi wanaopiga ni washamba tu kwa kuwa yeye hataki kulea mwanaume bali anataka kulelewa.
TUJIKUMBUSHE

KIJANA AMSAKA RAY C
SIKU chache baada ya nyota wa Bongo Fleva,
Rehema Chalamila, ‘Ray C’ kutangaza anatafuta mchumba, kijana
aliyejitambulisha kwa jina la Abubakar Ally ‘Babuu’ (21) amejitokeza
akisema yeye anataka ndoa na Ray C.
….Akigonga geti nyumbani kwa Ray C.
Babuu alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni Hospitali ya
Mwananyamala, Dar Kitengo cha Waathirika wa Madawa ya Kulevya
(Methadone) ambapo Ray C hufika kila siku kwa ajili ya dozi.
Ni baada ya kutonywa na vyanzo, mapaparazi wetu walifika eneo hilo na kumshuhudia kijana huyo akizuiwa kuingia hospitalini hapo na mlinzi.
…Akielekea ofisini kwa Ray C.
Mapaparazi wetu walifanikiwa kuzungumza naye ambapo alikiri kumsaka
Ray C kufuatia tangazo lake kwenye mtandao wake wa Instagram kwamba
anatafuta mwanaume wa kumuoa.
Babuu aliwaomba mapaparazi wetu wamuelekeze nyumbani kwa Ray C baada ya kumkosa kwenye Jengo la Biashara Complex, Mwananyamala.
“Mimi nataka kumuoa Ray C. Amesema kwenye tangazo lake Instagaram kwamba, mwanaume anayemtaka awe tayari kushea naye simu. Niko tayari, tena nitampa mapenzi yangu yote, nisaidieni kunielekeza kwake,” alisema Babuu.
Akaendelea: Nataka nimuoe. Mambo ya umri na pesa si vitu vya kuviangalia kwenye mapenzi.”
….Akigonga mlango wa ofisi ya Ray C.
Ilibidi mapaparazi wetu waongozane na kijana huyo hadi nyumbani kwa mwanadada huyo, Bunju, Dar
huku akiwa na mfuko mweupe ambao alidai ndani yake mlikuwa na barua ya posa na zawadi ya kadi.
Babuu aligonga geti kubwa, msichana mmoja alitoka na kujitambulisha kuwa ni ndugu wa Ray C. Alisema Ray C hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.
“Bado sijakata tamaa, nitamtafuta kila mahali hadi nimpate. Najua siyo rahisi, nimemtumia meseji na kumpigia simu lakini hapokei,” alisema Babuu.
Ray C alipotafutwa na Amani juzi kutaka kujua kama anafahamu alitafutwa alisema: “Siyo huyo tu. Wamenitafuta wengi sana. sikujua kama ishu itakuwa kubwa hivyo… Teh! Teh! Teh!”

Post a Comment