Mwana FA: Sitarajii kutoka kimataifa
Mwana FA wakati akihojiwa na Global TV Online leo.
FA akiitambulisha ngoma yake mpya iitwayo Sitoi Hela itakayoingia sokoni hivi karibuni.
Mwana FA akitoa baadhi ya vionjo vilivyomo katika ngoma yake ya Mfalme.
Mwana FA katika pozi mbalimbali na wafanyakazi wa Global Publishers Ltd baada ya mahojiano na Global TV Online.
MKONGWE wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ kwa mara ya kwanza
kupitia Global TV Online amefunguka kuwa hategemei kutoka kimataifa
kupitia muziki anaoufanya.
Akizungumza na Global TV kupitia Exclusive Interview, Mwana FA alisema kuwa wengi wanatoka na kukimbia kufanya kolabo na wasanii wa nje bila kutambua kuwa wanatakiwa kwanza watambulike nyumbani.
“Sina mpango na wala sitegemei kutoka kimataifa. Uwezo wa kufanya kolabo na msanii kama Chameleone wa Uganda ninano na nikisema nifanye kuwafurahisha mashabiki inawezekana lakini naangalia kufanya hivyo kutafanya muziki wetu ukue au ndiyo kusema ili mradi kusikika tu na Waganda,” alisema FA.
FA aliongeza kuwa kuna mwanamuziki wa Ghana, Sarkodie ambaye muziki wake umeweza kukubalika zaidi nchini kwao na nje ya nchi kutokana na kuchanganya lugha ya kwao na kiingereza.
“Mfano nchi kama Nigeria kwao kuna watu zaidi ya milioni 170 na nchini kwetu ni milioni 49 tu. Sasa kwa nchi kama ya kwao hata wakisema waimbe nyimbo kuwaimbia watoto wao watakubalika na wengi kuliko kwetu kwenye watu wachache.
“Watanzania wanatakiwa kuelewa kwanza tueneze lugha yetu ya kiswahili mfano kuna Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Congo na Burundi ambapo kote huko muziki wetu unakubalika na unaeleweka hivyo tufanye lugha ya Kiswahili iweze kukubalika zaidi kupitia nyimbo zetu na ndipo tuanze kukimbilia nchi nyingine,” alisema FA na kuongeza kuwa anatarajia kuachia ngoma akiwa na Marco Chali inayoitwa Sitoi Hela baada ya wiki mbili.

KUJUA ZAIDI KUHUSU MAHOJIANO HAYO, USIKOSE KUANGALIA GLOBAL TV ONLINE KUPITIA WWW.GLOBALTVTZ.COM
(PICHA/STORI NA ANDREW CARLOS/GPL)

Post a Comment