ad

ad

MSHINDO WA HIP HOP-TAARAB DAR LIVE IDD MOSI

Rais wa Manzese ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’.
Mwandishi Wetu
Dar es SalaamI
MESALIA wiki moja na siku kadhaa kufikia Sikukuu ya Idd Mosi ambapo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kutafuka moshi wa burudani kwa mastaa kibao wa muziki wa Hip Hop na Taarab kutumbuiza.

Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Juma Nature’.
Akizungumza na Championi Jumamosi, mratibu wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kuwa siku hiyo itakuwa ni zaidi ya burudani kwa wanaopenda burudani.
Abby Cool anasema, mtiririko wa burudani kutoka kwa wasanii utakuwa kama ifuatavyo;

Madee
Abby Cool anaanza kwa kumtaja, Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ kuwa naye ni miongoni mwa wasanii watakaokamua ndani ya ukumbi huo.
“Mara ya mwisho kwa Madee kufanya shoo ya kihistoria Dar Live ilikuwa miaka minne iliyopita na hii itakuwa mara ya pili na kifupi ni kwamba siku hiyo atakuja na ‘saprise’ kibao, hivyo mashabiki waje kumshuhudia.
Miongoni mwa ngoma zake atakazoimba ni Vuvula, Pombe Yangu, Ni Sheeda, Tema Mate Tuwachape na nyingine nyingi,” anasema Abby Cool.

Staa wa Ngoma ya Nimempata, Pamela Daffa ‘Pam D’.
Juma Nature
Mbali na Madee kuwakilisha Manzese, Abby Cool anasema usiku huo utapagawishwa pia na mkongwe mwenye historia katika muziki wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Nature’ ambapo ataendeleza historia ya kutimiza miaka 16 tangu aingie kwenye muziki huo.
“Temeke yote itahamia Dar Live kwani rais wao atakuwepo kuwapa ladha wanayoikosa kila mara.
“Mashabiki watarajie kumuona mkongwe huyu akipiga nyimbo zake zote kuanzia zile za zamani kama vile Ugali, Inaniuma Sana, Jinsi Kijana, Kighetogheto, Sitaki Demu pamoja na za hivi karibuni kama vile Kama Jana alioshirikiana na Lady Jay Dee, Komaa na nyingine nyingi,” anasema Abby Cool.

Jahazi
Kuonyesha kuwa utakuwa ni Mshindo wa Hip Hop- Taarab, kundi linalotikisa Bongo, Jahazi Modern Taarab litakuwepo maalum kwa  kuangusha nyimbo zao tisa zilizopo katika albamu yao mpya ya Mahaba Niue.
Abby Cool, alizitaja nyimbo hizo kuwa ni Mahaba Niue na Kaning’ang’ania Ng’ang’ani alizoimba Mzee Yusuf, Nina Moyo Sina Jiwe wa Leyla Rashid, Siumbuki wa Fatma, Nia Safi Hairogwi wa Mishi na nyingine kibao.

MSAGA SUMU
Bingwa wa nyimbo za Singeli, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ naye atakuwepo kuwaburudisha mashabiki wote wa muziki huo.
Miongoni mwa nyimbo zitakazowakosha mashabiki ni Historia ya Kweli, Napenda Simba na nyingine nyingi. Usiku huo pia Msaga Sumu atatambulisha kwa mara ya kwanza ngoma mpya aliyoshirikiana na Juma Nature inayoitwa Inaniuma Sana (remix).

PAM D
Staa wa Ngoma ya Nimempata, Pamela Daffa ‘Pam D’ naye atakuwepo kuweka historia katika kiwanja hicho.
Wimbo wa Nimempata alioshirikiana na Mesen umekuwa kama wimbo wa taifa kwenye klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi kutokana na kuwa na midundo ‘f’lani’ inayobamba kwa sasa.
Abby Cool anasema: “Mashabiki watarajie kuruka na midundo hiyo ambapo usiku huo Pam D atatambulisha wimbo wake mpya aliofanya na Christian Bella wa Popolipopo baada ya huu wa Nimempata.”

BURUDANI KWA WATOTO
Siku hiyo mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kabambe kwa watoto wote katika ukumbi huo sambamba na zawadi kibao.
“Tutakuwa pia na kundi namba moja kwa kutoa burudani kwa watoto la Masai Warriors, hawa wataonyesha michezo ya mazingaombwe, kukimbia kwa magunia, kugawa zawadi, sarakasi na michezo mingi.
“Mbali na Masai pia watoto watapata burudani ya kimuziki kutoka kwa kundi namba moja kwa kucheza la Wakali Dancers.
“Kila mtoto atakayeweza kucheza vizuri siku hiyo, atapata zawadi kabambe kutoka kwa Wakali Dancers.
“Wakali pia watawafundisha watoto staili mbalimbali za kucheza nyimbo za aina zote huku wengine wakipata burudani za bure zilizopo ndani ya ukumbi huo kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza na mingine mingi,” anasema Abby Cool.
Powered by Blogger.