MALAIKA: KWA PENZI LANGU, MAPEDESHEE WAJIPANGE
Mwanamuziki anayefanya poa, Diana Malaika ‘Malaika’ amefunguka kuwa wapo wanaume kibao wanaomtaka kimapenzi lakini kutokana na namna alivyoweka muziki mbele, mapedeshee hao wajipange sana kumnasa.
Akipiga stori na Ijumaa kuhusu maisha yake ya kimapenzi na usumbufu anaopata kutoka kwa wanaume wakware, Malaika alisema imekuwa ni ‘too much’ sasa maana wengi wamekuwa wakimsalandia wakidhani kwa vijisenti vyao watampata kirahisi.
“Watu hawajui tu ila ukweli ni kwamba mimi nimeweka muziki mbele kuliko kitu chochote, yaani hao mapedeshee wanaonitamani wajipange sana maana mimi siyo rahisi kama wale…” alisema Malaika.

Post a Comment