ESTER ADAIWA ANA ‘NGOMA’, AANGUA KILIO
Msanii wa filamu za Bongo, Ester Kiama
Msanii anayekuja kwa kasi katika anga la filamu, Ester Kiama amejikuta akiangua kilio kufuatia madai yanayoenezwa kuwa ana ‘ngoma’.
Taarifa ya ‘kuungua’ kwa staa huyo zimekuwa zikisambaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao ya kijamii huku mwenyewe akidai anasingiziwa na hivyo juzi kati akaamua kwenda kupima.
“Niliumia sana lakini ili kuwakomoa nikaenda kupima na majibu yakaonesha niko safi, nikajikuta nalia sana, si unajua inavyouma kusingizwa kitu? Sasa ili kuwakata kilimilimi hao wanaonizushia, majibu haya nitayabandika mtandaoni pia,” alisema Ester.
HABARI NA Imelda Mtema - GPL

Post a Comment