Davina yamemkuta amedaiwa kutoswa na bosi wake aliyevunja ndoa yake!
Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya 'Davina'.
Waandishi wetu Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya amedaiwa kutoswa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe ambaye alikuwa bosi wake kwenye kampuni moja iliyopo Kinondoni jijini Dar, Ijumaa limetonywa kila kitu. Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, baada ya Davina kuzinguana na mumewe kisa kikiwa ni bosi huyo (Jina tunalihifadhi kwa sasa) alifunguliwa ofisi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kisha maisha yakaendelea.
” Davina anasemaje? Davina alipovutiwa waya na kuulizwa juu ya madai ya kutoswa na mwanaume aliyevunja ndoa yake alisema amechoshwa na maneno ya watu kwani hajawahi kuwa na uhusiano na bosi wake huyo. “Mh! Watu wananitungia habari jamani mimi sipendi kwa sababu hawajui tu wanavyoniharibia, sijawahi kuwa na uhusiano na bosi wangu, kuhusu kazi mbona bado naendelea na hivi ninavyokwambia naelekea hapo kazini,” alisema Davina.
Anapingana na Mike Sangu Akizungumzia ishu hiyo, Mike Sangu aliyekuwa akifanya kazi ofisi moja na Davina alisema: “Hayo mambo ya Davina kuwa na uhusiano na mkurugenzi wetu siyajui, ninachojua kwa sasa tumesimama kidogo kwa sababu tunafanya usaili wa watu ili tufungue televisheni kwa ujumla kwani mwanzo ilikuwa TV Online na hata huyo Davina tumemuambia alete CV,” alisema Mike.
DAVINA AMWANGUKIA MUME WAKE ===>BONYEZA HAPA
CHANZO: GPL

Post a Comment