Chadema yaahidi kutangaza mgombea urais wa Ukawa wakati muafaka utakapowadia
Chama
cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) na vyama washirika vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA ) wamesema kuwa wako imara na
wamejiandaa vyema kushinda katika uchaguzi mkuu ujao kwa kukiondoa
madarakani chama cha mapinduzi, licha ya kauli inayodaiwa kutolewa na
katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye wakati wa ziara ya katibu mkuu
wa chama hicho mkoani Mwanza kwamba CCM itashinda hata kwa goli la
mkono.
Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
viwanja vya magomeni kirumba jijiji Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya
wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo katika mkutano huo mwenyekiti
wa taifa wa Chadema Mh.Freeman Mbowe amewatambulisha rasmi waliokuwa
wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Mh. James Lembeli na Mh.
Esther Bulaya ambao wamehamia Chadema, huku akiwatahadhalisha wagombea
wa nafasi za udiwani na ubunge kutokubali kununuliwa kwa lengo la
kukihujumu chama hicho.
Awali mwenyekiti wa taifa wa baraza la wanawake wa Chadema
(BAWACHA) Halima Mdee, naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa
Zanzibar Salum Mwalim pamoja na mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu
wamesema wakati umefika kwa watanzania kuchagua viongozi wanaokubalika
na wenye uchungu na raslimali za taifa kwa uhuru bila kutishwa kwani saa
ya ukombozi kupitia sanduku la kura utajulikana oktoba 25 mwaka huu.
Kwa upande wao waliokuwa wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi
James Lembeli wa jimbo la Kahama na Esther Bulaya viti maalum umoja wa
vijana CCM mkoa wa Mara nao wametumia mkutano huo kueleza
kilichowasukuma kujiunga na Chadema.

Post a Comment