AZAM FC YAKOMAA, YATINGA FAINALI KAGAME, INAKUTANA NA GOR MAHIA
Fainali
ya Kombe la Kagame sasa itakuwa ni Azam FC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.
Azam
FC imekuwa ya pili kuingia fainali kwa kuitwanga KCCA kwa bao 1-0 huku
Gor Mahia ikiwa imetangulia baada ya ushindi dhidi ya timu ngumu ya Al
Khartoum.
Hii
ni mara ya pili kwa Azam FC kuingia fainali ya Kagame, mara ya kwanza
ikiwa ni 2012 ambapo ilifungwa na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Tom
Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.
Mechi ya fainali itachezwa Jumapili, ikitanguliwa na ile ya mshindi wa tatu kati ya KCCA dhidi ya Al Khartoum.
Post a Comment