ad

ad

WATU LAKI TANO WAJITOKEZA KUWAPOKEA MABINGWA WAPYA WA NBA, MAREKANI

 
Mitaa ya mji wa Oakland ilikuwa imefurika watu baada ya mabingwa wapya wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kuwasili.

Mashabiki wanaofikia 500,000 au zaidi walijitokeza kuwapokea Golden State Warriors ambao hawakuwahi kulichukua kombe hilo kwa miaka 40.
Mmoja wa watu maarufu alioungana na wengine ni rapa maarufu na mkongwe MC Hammer.
Wakali hao walishinda kombe hilo baada ya kuwashinda Cleveland Cavaliers waliokuwa wanaongozwa na mkali LeBron James.





No comments

Powered by Blogger.