USAJILI: AZAM YAWARUHUSU WACHEZAJI WAKE WALIOMALIZA MIKATABA
Amri Kiemba.
Gaudence Mwaikimba (kushoto) ambaye ni mmoja wa wachezaji walioruhusiwa kutafuta timu.
Azam FC imewaruhusu wachezaji wake watatu waliomaliza mikataba yao
kutafuta timu nyingine. Wachezaji hao ni Gaudence Mwaikimba, Amri Kiemba
(mkopo toka Simba) na Wandwi JacksonPia klabu imerefusha mikataba ya wachezaji waliokuwa wakikaribia kumaliza mikataba yao. Wachezaji hao ni Said Morad, Erasto Nyoni, Dedier Kavumbagu, Khamis Mcha, Waziri Salum, Brison Raphael, Joseph Kimwaga, Mudathir Yahya na Farid Mussa.
Taarifa hii imetolewa leo katika ukurasa wa Facebook wa klabu hiyo ambayo imesema hadi sasa bado haijaingia mkataba na mchezaji yeyote kutoka nje ya nchi.
Post a Comment