TRA YAZITAKA SIMBA, YANGA NA AZAM KUWALIPIA KODI WACHEZAJI, MAKOCHA
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya
nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi
kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Kamshina
wa TRA ameliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa katibu
mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri
walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka
kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri.
Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba yao kugongwa muhuri na stempu.
Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba 7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.
Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.
Miongozi mwa timu zenye kuingia MIkataba na wachezaji na makocha nchini ni Azam FC, Simba na Yanga SC.

Post a Comment