ad

ad

JAMANI DADA MARTHA...LOOH! - 4

 

ILIPOISHIA
 “Nimejilaza kitandani tayari kwa kusinzia. Wewe je?”
“Hata mimi nimelala my bro...”
“Umelalaje hapo kitandani my sweetheart sista? Please niambie...”
TAMBAA NAYO MWENYEWE...
“Nimelala chali au niseme nimelala naangalia juu.”
“Umejifunika shuka?”
“Hapana my bro! Na joto lote hili? Wewe je?”
“Mimi nimelala naangalia chini, yaani tumbo limegusa godoro, tofauti na wewe mgongo ndiyo umegusa godoro.”
“Duu! Tumebadilishana, mimi naangalia juu wewe unaangalia chini...teh! teh!”
“Kumbe tumelala vizuri sana. ndiyo inavyotakiwa, mwanaume analala hivyo na mwanamke analala hivyo kama wewe.”
“Teh! Teh! Mi nalala bwana kaka, kesho.”  “Kabla hujalala nataka nikuombe kitu kimoja sista...”
“Kipi hicho braza?”
“Kesho tukutane lakini iwe sehemu ya siri sana.”
“Sehemu ya siri kama ipi bro? Unanitisha.” “Kama hotelini.”
“Mh! Jamani kaka! Hotelini tena? Yaani chumbani au?”
“Yes!”
“Ah! Sasa itakuaje mtu na kaka yake chumbani? Inawezekana kweli?”
“Mimi naweza sana.”
“Mimi siwezi kaka.”
“Kwa nini huwezi dada?”
“We unajua ni vigumu. Unaweza kuzidiwa ukanibaka bure, sitaki.”
“Yaani sikia sista...tukiwa mle hatutakaa pamoja, wewe kona nyingine na mimi kona nyingine. Halafu kila mmoja atakuwa ndani ya mavazi...”
“Lakini kisa cha yote hayo ni nini?” aliuliza Liz...
“Sikia Martha...”
“Nilisema usiniite Martha, niite Liz.”
“Oke. Sikia Liz...hakuna kisa ila nimependa tu. Isitoshe mimi na wewe ni mtu na dada yake, siwezi kuwaka tamaa kama ambavyo najua na wewe hutaweza kuwaka tamaa.”
“Mh! Una maneno matamu sana bro! Haya sawa, lakini asitokee mtu akakiuka.”
“Hatutaweza sista bwana.”
“Sawa. Usiku mwema basi, kesho my kaka.”
“Lala salama my sista.”
Liz alipanda kitandani huku akiwa na maswali kibao kuhusu ombi la Roi kwamba kesho yake wakutanie chumbani hotelini...
“Hivi amekusudia nini? Au anataka kuonesha kwamba, hata tukiwa chumbani wawili hatuwezi kuzini kwa vile tumeshakuwa kaka na dada? Anyway, tutaona hiyo kesho,” aliwaza Liz na kupitiwa na usingizi.
Kwa Roi hali ilikuwa hiyohiyo, naye aliwaza...
“Lakini si naweza kabisa...naingia naye hotelini, chumbani lakini sifanyi naye chochote...mwenyewe atashangaa sana.”
***
Kulikucha, Liz ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtumia meseji Roi...
“Morning my bro...”
Roi alifurahi sana kuamshwa na Liz, akamjibu...
“Morning my sista...umeamkaje?”
“Nimemka salama bro...wewe?”
“Hata mimi pia.”
“Oke, kumekucha.”
“Ni kweli sista...sasa vipi ile safari yetu?”
“Saa ngapi?”
“Nataka iwe mchana wa leo.”
“Utaniambia ni wapi!”
“Poa sista.”
“Lakini bro, ni kweli hutafanya lolote kwangu?”
“Ni kweli kabisa sista, wala usiwe na shaka.”
“Basi sawa.”
***
Ilikuwa saa saba mchana, Roi alimtumia meseji Liz ya kumshtua kwa ajili ya kumfuata alipo...
“My sweetheart sista...”
“Honey bro!”
“Sasa?” “Nakusikiliza wewe kaka’angu mpenzi.”
“Mimi nipo hapa Kisasa Hotel, Kinondoni. Njoo basi.”
“Duu! Bro uko shap sana! umeshatafuta na hoteli kumbe? Poa nakuja sasa hivi.”
Roi alikuwa ndani ya chumba cha hoteli hiyo. Mwili ulimtetemeka kila mara. Alianza kuhisi kwamba, kiapo chake kwa Liz si cha kweli...
“Hivi nitaweza kweli kukaa naye mpaka mwisho bila chokochoko?” alijiuliza.
Dakika kumi na tano mbele, Liz alimpigia simu kwamba amefika yuko nje...
“Njoo mpaka ndani sista, utaoneshwa chumba nilichopo. Ni namba hamsini.”
“Poa bro.”  Mara mlango uligongwa, Roi akaruhusu mtu kuingia, Liz akazama ndani...
“Oohooo! Huyu mchokozi sasa,” alisema moyoni Roi baada ya kumwona Liz amevaa suruali ya matirio kama t-shirt, mbaya zaidi imembana vilivyo na juu kiblauzi chepesi mpaka unaona ramani ya kifua chote.
“Karibu sana sista,” alikaribisha Roi.
Liz aliweka kipochi chake kwenye meza kisha akakaa upande wa miguuni mwa kitanda na kuangalia ukutani wakati Roi alikaa eneo la kichwani naye akiangalia ukutani...
“Za hapa?” alisalimia Liz...
“Poa sista, za safari?”
“Njema tu. Ndiyo umeamua kweli kabisa kuchukua chumba kaka jamani?”
“Usijali sista, hili ni eneo salama sana kwetu.”
“Mh! Mfano akija mtu akauliza sisi ni akina nani tukasema ni mtu na kaka yake itakuaje? Ataamini kweli bro?”
“Nani kwanza atakuja sista?”
“Mfano yaani bro...”
“Hamna cha mfano sista, hakuna atakayekuja humu ndani.”
Walianza maongezi ya mbali kwa mbali, kila mmoja akiangalia ukutani. Mwishowe Liz alilala chali, nusu ya mwili kuanzia kiunoni kwenda juu kitandani, nusu iliyobaki ikining’inia chini...
“Umechoka nini sista?” aliuliza Roi...
“Nahisi kusinzia bro...”
“Hata mimi pia,” alisema Roi na kulala kama alivyolala Liz, wakakutana vichwa!
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma chombezo hili tamu sana

No comments

Powered by Blogger.