TAIFA STARS YAFUNGWA NA UGANDA 3-0
MABAO mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu yanaweza kuwa yamehitimisha historia ya kocha Mholanzi, Mart Nooij katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kufungwa 3-0 na Uganda usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo wa kwanza Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Rwanda mwaka 2016, Sekisambu alimtungua kipa Deo Munishi ‘Dida’ bao moja kila kipindi, wakati bao la tatu lilifungwa na Farouk Miya dakika ya 89.
Post a Comment