NISHER KUFANYA MAPINDUZI SOKO LA VIDEO BONGO
MTAYARISHAJI wa video za muziki anayefanya vizuri Bongo, Nisher David, hivi karibuni amedai kuwa yupo mbioni kufanya mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya video za muziki wa Kibongo ikiwa ni pamoja na kufanya video na wasanii wa kimataifa.
Akichonga na Centre Spread, muandaaji huyo ambaye ni miongoni mwa madairekta wakubwa nchini aliwataja wasanii anaotarajia kufanya nao kazi mapema mwezi ujao kuwa wanatoka nchi za Rwanda, Ethiopia na Nigeria huku akidai muda ukifika ataweka wazi majina yao.
“Zaidi ya hilo, mwezi Julai nategemea kutembelea nchi mbalimbali duniani kutafuta soko la kazi zangu. Watanzania, hasa mashabiki wanaofuatilia kazi zangu wajiandae kumuona Nisher mwingine ambaye anakuja kubadilisha soko la Video Bongo,” alisema Nisher ambaye pia amewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa nchini akiwemo Fid Q, Joh Makini, G Nako, Belle 9 na wengine wengi.
Post a Comment