MSANII BONGO MUVI AIKIMBIA NYUMBA KISA MAUZAUZA!
Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
MAJANGA! Msanii
wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ amejikuta akifungasha virago na
kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Kinondoni jijini Dar
kutokana na mjengo huo kutawaliwa na mauzauza yanayosadikiwa kuwa ya
kishirikina.
Chanzo
makini kilicho jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mwanadada huyo
kilieleza kuwa, baada ya kuvumilia vimbwanga vya kishirikina ameamua
kuondoka.
“Hii
nyumba wapangaji huwa hawadumu kwa kushindwa kustahimili wanayoyaona
sijui ina balaa gani, tunashangaa yeye ameweza kukaa kwa mwaka mzima na
kuvumilia majanga yote, inataka moyo.
“Sasa
leo uzalendo umemshinda baada ya mpangaji mwenziye kufariki ghafla wiki
iliyopita, ambapo siku moja kabla ya kifo chake alipambana na paka
aliyekojoa mlangoni, tangu itokee hiyo ishu amekuwa akija hapo
kuchungulia nyumba na kuondoka, leo kaona isiwe tabu, anahamisha vitu
vyake,” kilisema chanzo.
Baada
ya kupata fununu hizo bila kupoteza muda wadakuzi wetu waliibuka
nyumbani kwa msanii huyo na kumkuta akiwa kwenye hekaheka ya kuhama na
kukiri kuwa amelazimika kufanya hivyo kutokana na aliyokuwa akiyaona
kwenye nyumba hiyo.
“Kuna
muda nikiwa chumbani nasikia taa zinawashwa na kuzimwa nikitazama sioni
mtu, wakati mwingine paka anakuja chumbani na kucheza kwenye kioo
ukimfukuza na kufunga mlango dakika chache unamuona tena na cha
kustaajabisha nakuwa najiuliza amepita wapi sipati jibu, kwa ujumla
nyumba hii ina mauzauza kibao ambayo nimeshindwa kuyavumilia, hali ni
mbaya nahamia kwa rafiki yangu,” alisema Bozi.




Post a Comment