MOAT yakomalia muswada wa habari
Mwenyeki wa MOAT Dk. Reginald Mengi
WAKATI Serikali ikiendelea kuweka
vikwazo na kutaka kupitisha muswada wa vyombo vya habari kwa nguvu,
Wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania (MOAT), wamesema wanauhakika
kwamba hautapitishwa Bungeni pasipokujadiliwa upya.
Aidha, imebainika, Serikali imeondoa kinyemela Muswada wa vyombo vya habari katika Bunge linaloendelea hivi sasa na kupenyeza muswada mwingine wa sheria ya upatikanaji wa habari.
Akizungumza katika mkutano wa MOAT
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyeki wa MOAT Dk. Reginald
Mengi amesema, muswada huo haujakubalika kwani bado unakandamiza
waandishi wa habari.
Mengi amesema sheria ya upatikanaji wa
habari bado itawanyima uhuru wa usambazaji wa habari kwa vyombo
vinavyomilikiwa na watu binafsi ambalo ni kinyume cha katiba ya nchi.
“Kinachoshangaza ni kwanini serikali
inazidi kutunga sheria ambazo kwa upande mmoja inabana? Wakati ibara ya
5 kifungu cha (1) kinasema kila mtu anahaki ya kupata taarifa
iliyochini ya wenye taarifa na kwamba kila mwenye taarifa atatoa taarifa
ambayo ipo chini ya mamlaka yake” amesema Mengi.
“Sheria hizi bado zinamkanganyiko mkubwa
hazieleweki upeo wa serikali hii kwa upeo wangu serikali inajaribu
kuuzima uhuru wa kukusanya na kusambaza habari kwa wananchi” amesema
Mengi.
Amesema endapo muswada huo utapita nchi
hii itakuwa katika hatari ya kupata habari zisizorasmi, kutokana kwamba
watoa habari hawatakuwa huru.
Nae Rostam Aziz mmoja kati ya wajumbe wa
MOAT ameisisitiza Serikali kutopeleka muswada huo bungeni unaweza
kuleta sheria mbaya nchini na kandamizi.
“Sisi kama MOAT tunatamka sauti moja
kwamba tutahakikisha muswada huu hautapitapitishwa hadi serikali
itakapoamua kurudi nyuma na kutushirikisha wadau wote ndipo
utapitishwa.”. amesema Rostam.

Post a Comment