AZAM YAWACHAPA PRISONS BAO 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI FA CUP
Azam FC imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuichapa Prisons kwa mabao 3-1.
Katika
mechi tamu na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es
Salaam, timu zilionyesha upinzani mkubwa katika kipindi cha kwanza.
Ulikuwa
ni upinzani mkali kati ya timu hizo mbili lakini Azam FC ndiyo
waliokuwa makini kuzitumia nafasi walizozipata kupitia Shomari Kapombe
aliyefunga mabao mawili na Hamis Mcha aliyefunga moja.
Jeremiah
Juma ndiye alifunga bao pekee la Prisons ambayo kila muda ulivyokuwa
ukisonga mbele ilionekana kupoteza kasi na umakini.
Azam FC inakuwa ni timu ya tatu kutinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya Mwadui FC na Yanga.
Post a Comment