JAMANI DADA MARTHA...LOOH! - 3

ILIPOISHIA
Roi alimpa simu yake mhudumu mmoja wa baa hiyo aende nayo barabarani...
“Ukifika pale piga namba hii, utakutana na dada mgeni wangu mmoja mlete hapa,” alisema Roi, mhudumu akaondoka na simu.
Baada ya dakika mbili, mhudumu aliongozana na Martha mpaka alipokaa Roi na marafiki zake. Kazi ikawa, Martha akae wapi sasa? Akae kwenye kiti cha jirani na kaka yake, Roi au?
GALAGALA NAYO MWENYEWE...
“Karibu hapo,” alisema Roi akimtengea kiti Martha ili akae jirani na yeye.
Martha siku hiyo alivaa suruali ya jinzi iliyomkaa sawasawa kwa kumbana, alionekana ni mwanamke mwenye kujiamini sana. Ongea yake, tazama yake ilimfanya kila mmoja kati ya Roi mwenyewe, Pauli na Julio kujua kuwa, Martha ni mwanamke...
“Bro,” Martha alituma meseji palepale kwenda kwa Roi...
“Sema sweet sista.”
“Mimi nina majina mawili. La kwanza, Martha. La pili ni Liz. Lakini jina ambalo limezoeleka sana ni Liz. Kwa hiyo kuanzia leo nitapenda uniite Liz na achana na jina la Martha.”
Roi alipoisoma meseji hiyo aliona sawasawa tu. Atumie jina la Martha, atumie la Liz sawa, kwake majina yote yalikuwa ni mazuri...
“Poa sista, love u sana...”
“Love u too.”
Mazungumzo kati ya Roi na marafi zake yaliendelea huku Liz akiwa ametulia kimya pembeni kwenye kiti akiwasikiliza. Ilifika mahali, Roi akawaomba watulie ili atoe utambulisho...
“Jamani...jamani...” Roi alisema kwa maana ya kuomba utulivu...
“Sema kaka...”
“Huyu anaitwa Liz, ni dada yangu kipenzi,” alisema Roi huku akimshikashika begani dada yake huyo...
“Kumbe hapa Dar upo na dada yako? Sisi tulikuwa hatujui,” alisema Julio...
“Hata mimi nimeshangaa sana,” alidakia Pauli huku wote wakimkaribisha Liz tena na tena...
“Asanteni jamani, nashukuru sana.”
Baada ya utambulisho huo, mazungumzo ya wote yalikata, sasa ikawa wote wako na simu zao. Kila mmoja alituma meseji alikokujua yeye...
“Bro!” alituma Liz kwa Roi...
“Yes, niambie...”
“Upo oke?”
“Nipo sawa mama, wewe?”
“Hata mimi my bro. Nipo happy kuwa na wewe.”
“Wewe kama mimi.”
“Kumbe tuko sare!”
“Umeona ee?”
“Yes! Sijakuboa lakini?”
“Wala! Hujaniboa! Hivi sista wewe ni mwenyeji wa wapi?”
“Natokea Iringa bro.”
“Oke...oke...kamwene,” alitania Roi...
“Kamwene...”
“Mnogage?”
“Ndi mnofu...Teh! Teh! Teh! Sijakaa sana Iringa lakini nakijuajua bro...teh!”
Roi naye alimrudishia meseji kwa kicheko huku akimchombezea kwa maneno kama...
“Umependeza sana my darling sista...”
“Hata wewe sweetheart bro.”
Walikunywa, walikula, ikafika mahali Liz akaamua kuaga kwa Roi kwa njia ya meseji...
“Baby bro, mimi naondoka zangu.”
“Mh! Mara hii sista?”
“Usijali, siku nyingine tutakaa wote kwa muda mrefu sana.”
“Basi poa.”
Roi alisimama, Liz naye akasimama, akawaaga Pauli na Julio, Roi akamsindikiza hadi barabarani kwa ajili ya kupanda daladala.
Walisimama kando ya barabara, Roi akapeleka mdomo wake pembeni mwa shavu la Liz, akambusu...
“Mmmwaaa....”
“Thanx my bro, usiku mwema, tutachati,” alisema Liz...
“Poapoa.”
Roi alirudi kuungana na marafiki zake, Julio na Pauli...
“Ee bwana naona sista kama hajayazoea mazingira haya,” alisema Pauli...
“Ni kweli, amesema pana kelele sana.”
“Lakini jamani ni kweli. Mnajua kukaa hapa panataka moyo maana hakuna utulivu. Kama umetoka kazini na unataka kupumzika, si mahali pazuri sana.”
“Ni kweli kabisa,” alidakia Julio...
“Ni kweli,” alidakia Roi mwenyewe sasa.
***
Liz alipofika nyumbani kwake, alimtumia meseji Roi kwamba amefika...
“Bro, nimefika. Leo nimefurahi sana kukutana tena na wewe.”
“Hata mimi...”
“Oke, nataka kuoga kwanza halafu baadaye tutaendelea kaka yangu.”
“Usijali dada yangu Martha.”
“Bro! Nilikwambia tumia Liz na siyo Martha.”
“Ha! Nilisahau sista jamani! Oke dada Liz...”
Roi na wenzake waliendelea kunywa, wakanywa wee! Wakanywa mpaka kila mmoja akaanza kuonesha dalili kwamba amelewa...
“Jamani vipi? Suni tunatimua?” Julio aliwasilisha hoja binafsi...
“Ni kweli,” alishadadia Pauli...
“Sawasawa,” alimalizia Roi.
***
Usiku wa saa tano, Roi alikuwa kitandani, alilala chali akiwa ndani ya bukta tu. Alikuwa ameingia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuangalia nini kinaendelea. Mara meseji kwenye WhatsApp ikaingia...
“Baby...” ilitoka kwa Liz, Roi akashangaa kuona meseji ya Baby imeingia bila nyongeza. Alizoea baby bro, sweetheart bro na mengineyo...
“Darling,” na yeye alitingisha kiberiti, akatuma meseji hiyo bila kuongezea neno sista...
“Umeshatoka hapo?”
“Zamani sana sista, niko home.”
“Unafanyaje muda huu?”
“Nimejilaza kitandani tayari kwa kusinzia. Wewe je?”
“Hata mimi nimelala my bro...”
“Umelalaje hapo kitandani my sweetheart sista? Please niambie...” Je, unajua nini kilitokea hapo?
Post a Comment