BAND YA MUZIKI WA DANSI INAYOTIKISA BONGO KWA SASA, RUBY BAND YATIKISA
BAND ya muziki wa Dansi inayotikisa Bongo kwa sasa, Ruby Band leo imetikisa ndani ya Global TV Online katika kipindi cha Exclusive kwa kuimba ‘live’ nyimbo zao karibu zote.
Band hiyo inayobamba na Wimbo wa Kisebusebu, iligeuka kuwa kivutio ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar kwenye studio za Global TV Online pale walipoimba akapera wimbo wao wa Noma na kuwafanya wengi waliowatizama kuwafananisha na makundi ya muziki wa Dansi ya nchini Kongo.
Band hiyo inayoongozwa na Ruby inaundwa na vichwa vinne ambavyo ni Ismail Yahya ‘Suma Lay’, Sunday Mtore ‘Cmyner’ Khalid Waziri ‘Kwea’ pamoja na Laurence Clement ‘Maya.’
(PICHA: GLOBAL TV ONLINE)
Post a Comment