ad

ad

MAN UTD YAMALIZANA NA KIUNGO ILKAY GUNDOGAN WA BORUSSIA DORTMUN


Kwa mujibu wa gazeti la Goal, kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan (pichani) amekubaliana maslahi binafsi na Manchester United tayari kwa usajili wa kwenda Old Trafford mwezi ujao.
Gundogan, 24, tayari alishatangaza kuwa hatarefusha mkataba wake Dortmund lakini ada baina ya klabu hizo mbili bado haijafikiwa.
Kocha wa United Louis van Gaal wiki iliyopita alikiri kuwa anatafuta kiungo mchezajishaji kwaajili ya dirisha la usajili la kiangazi.
Boss huyo wa United alisema: "Namba 6 ni sehemu muhimu katika timu. "Nina maeneo mengi ntakayoboresha na namba 6 ni mojawapo."
Man Utd reportedly agree deal for Borussia Dortmund ace Ilkay Gundogan
DILI LIMEKUBALI? imeripotiwa kuwa Manchester United imekubaliana na Ilkay Gundogan 
“Sina mchezaji mwingine wa dimba la kati kama Michael Carrick”
Louis van Gaal
"Unaweza kuona msimu huu, kwa mfano Michael Carrick akiiumia nakuwa sina chaguo lingine, ninae Ander Herrera na anacheza vizuri lakini sio eneo lake rasmi.
"Pia nimelazimika kumchezesha Wayne Rooney, lakini nae hiyo si sehemu yake uwanjani.
"Nimekuwa nikifanya hivyo kwasababu sina kiungo mwingine mkabaji kama Carrick na ndio maana eneo hilo lazima niliwekee kipaumbele msimu huu".
Dortmund tayari imemsajili Gonzalo Castro kutoka Bayer Leverkusen kama mbadala wa Gundogan. 

CHANZO: SALUTI5.COM

No comments

Powered by Blogger.