MAIMARTHA AMUUMBUA SAJENT
Kumekuwa na madai kuwa, mwanadada Husna Sajent ameolewa na msanii
mwenzake wa filamu, Salim Ahmed ‘Gabo’ lakini wenyewe wamekuwa
wakikanusha! Hata hivyo, juzikati Maimartha Jesse ‘Mai’ alimwaga mchele
mbele ya kuku kwa kumuita Husna ‘Mrs Gabo’.
Katika utambulisho huo, Mai alimuita Husna ‘Mrs Gabo’ akimaanisha na si kwa utani, hali iliyowafanya watu kuanza kunong’ona kwa chini na kumuacha Husna akicheka asijue namna ya kuua soo.
Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mai alifanya hivyo pale alipokuwa akiwatambulisha mastaa
waliohudhuria sherehe ya ‘baby shower’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika
Mwendopolepole, Bagamoyo mkoani Pwani.Katika utambulisho huo, Mai alimuita Husna ‘Mrs Gabo’ akimaanisha na si kwa utani, hali iliyowafanya watu kuanza kunong’ona kwa chini na kumuacha Husna akicheka asijue namna ya kuua soo.
Msanii wa filamu za Kibongo, Husna Sajent.
“Si mwenyewe anasema ile picha iliyovuja akionekana kafunga ndoa na
Gabo ni filamu, sasa kumbe watu wake wa karibu wanajua ukweli, mh!
Makubwa,” alisikika akisema dada mmoja aliyekuwa eneo hilo la sherehe.
Post a Comment