MADRID YATUPWA NJE UEFA: MATOKEO REAL MADRID 1-1 JUVENTUS (AGG 2-3)
MSHAMBULIAJI kinda wa umri wa miaka 22 wa kimataifa wa Hispania, Alvaro Borja Morata Martin ameivua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya timu yake ya zamani, Real Madrid.
Morata ameifungia bao Juventus katika sare ya 1-1 na Real leo Uwanja wa Bernabeu katika Nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa. Juve sasa inasonga mbele kwa ushindi wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 mjini Turin.
Post a Comment