ISHU SIYO KUPEWA MIMBA, ANAYEKUPA NI NANI, WAKATI GANI?-2
BILA shaka mpenzi msomaji wa safu hii u-mzima wa afya. Tunakutana
tena katika eneo letu maridhawa la kupeana elimu ya uhusiano.Kwa wale
tuliokuwa pamoja, wiki iliyopita tuliianza mada iliyopo hapo juu. Mada
hii ilikuwa na lengo la kuwataka wanawake wawe makini katika suala zima
la kutaka kuzaa.
Nilisema
hatari anayoipata mwanamke asiyemjua vizuri mwanaume ni pamoja na
kukubali kuwa mwanamke wa kuzugia. Yeye anachoangalia ni kusaka mimba
bila kujali amefanywa ‘kidumu’. Kweli anayekufanya wa kuzugia anaweza
kukupa mimba lakini baadaye anakuacha na kumuoa yule
ampendaye.ENDELEA...
Ukishaachwa solemba utahamia kwa mwanaume mwingine ambaye naye pengine mambo yanakuwa ni yaleyale.
Hiyo ndiyo itakuwa aina ya maisha unayoishi. Leo kwa huyu, kesho unahamia kwa mwingine.Hivyo basi, ni vyema ukaanza kujitengenezea mazingira mazuri mapema ili utakapofika wakati uolewe na muweze kufika katika hatua nzuri ya kuzaa na yule ambaye atakuwa na manufaa kwako.
Ukishampata mtu ambaye ni sahihi, tengeneza mazingira ya kujua kwamba ni muda gani na wewe unatakiwa kuzaa. Hapo ina maana tayari huyo uliyenaye muwe mmeshazungumza na kufikia muafaka wa kufunga ndoa.Achana na tafsiri ya kusema ‘acha nile kwanza ujana, nitazaa baadaye.’ Muhimu kuwa na mtu sahihi, kupanga mipango sahihi ya ndoa na kisha kuzaa na mtu sahihi katika muda muafaka.
Usikubali kucheza na ujana, kujifanya unakwenda na fasheni kila kukicha, eti huoni haja ya kuwa na mtu wa moja kwa moja kulingana na matakwa yako.Mfumo wa maisha yako utakuwa hauna njia maalum, matokeo yake utakuja kushtuka tayari umri umekutupa mkono na kuona huna uwezekano na kuolewa tena, kinachofuata hapo ni kutafuta mimba kwa lazima.
Umri ukishakupa kisogo huwezi tena kuangalia anayekupa mimba ni nani. Mbaya zaidi unaweza kukubali kumbebea huyu mimba, akakuacha, ukambebea mwingine naye akakuacha vilevile.Matokeo yake utakuwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawana baba maalum. Wote wamekuzalisha na kukukimbia. Malezi ya watoto yanakuwa kwako.
Zaidi utakachoambulia hapo ni majuto. Kila ambaye utakuwa unampa pendo lako, analitupa na kuendelea mbele na maisha yake mengine.Utajuta na kujilaumu kwamba kwa nini usingejipanga mapema. Muda unakuwa haukuruhusu tena, huo ndiyo unakuwa ni mustakabali wa maisha yako.
Mwanamke anayetaka kuishi maisha yenye thamani ya ndoa, anapaswa kujitambua mapema. Anapaswa kujua aishi vipi ili asitumike kisha kuachwa solemba.Furaha ya watoto inakamilika kama wanakuwa na baba wa uhakika. Watoto wapate malezi ya pande zote mbili, baba na mama.Ukichanga karata zako vibaya, utaishia kuzalishwa watoto wengi wasiokuwa na baba maalum, achilia mbali kupata magonjwa.

Post a Comment