ad

ad

YANGA YAIFUNGA MBEYA CITY BAO 3-1 TAIFA DAR



Magoli 3 - 1 ya timu ya Yanga Sc ya mtaa wa Jangwani yametosha kuizamisha timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ulichezwa jioni ya leo katika dimba la uwanja wa taifa.
1 - 0 mchezaji wa kigeni kutoka Liberia Kper Sherman alifunga goli dakika ya 18 akimalizia mpira wa Amis Tambwe.
2 - 0 kiungo Salum Telela akafunga tena goli la pili kwa mpira ulioanzishwa na Haruna Niyonzima dakika ya 37 ya mchezo.
2 - 1 Themi Felix akawapatia wageni goli dakika ya 39 kabla ya kwenda mapumziko.
3 - 1 kapteni Haroub Canavaro alifunga kwa kichwa goli la dakika ya 50 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mjanja Niyonzima.
Yanga sasa wanaendelea kuwepo kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara kwa pointi nane zaidi mbele ya wapinzani wao wa karibu Azam Fc.

No comments

Powered by Blogger.