Uchaghuzi Mkuu upo pale pale – NEC
HATIMAYE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekata mzizi wa fitna. Insema kuwa
haina mpango wowote na wala haikusudii kuahairisha uchaguzi mkuu ujao
Oktoba mwaka huu, kutokana na sababu yoyote ile kama ambavyo inadaiwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Kauli ya NEC inaondoa hofu iliyotanda kwa vyama vya siasa, kwamba baada ya kushindwa kufanya kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa 30 Aprili mwaka huu, sasa inatengeneza mazingira ya kumwongezea muda Rais Jakaya Kikwete kwa kisingizio cha kutokamilisha uandikishaji wa wapiga kura.
Akizungumzia
mwenendo mzima wa uandikishaji wa wapiga kwa mfumo mpya wa Biometric
Voters Registratin (BVR) unaoendelea mkoani Njombe, Mwenyekiti wa NEC,
Jaji mstaafu Damian Lubuva, amewaambia waandishi wa habari kuwa “hadi
sasa tayari tumepokea BVR Kits 248.”
Amesema
“NEC ilianza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga katika mkoa wa
Njombe 16 Machi, 2015, na sasa uandikishaji huo utakamilika rasmi 18
Aprili mwaka huu.”
Kwa
mujibu wa Jaji Lubuva, uandikishaji huo, umefanyika kwa mafanikio
makubwa katika kata zote za halmashauri ya wilaya ya Njombe Mjini na
Vijijini, Wanging’ombe, Ludewa, Makete na Makambako.
Amefafanua
kuwa, pamoja na kuahirisha kwa tarehe ya kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa, NEC inaendelea na uandikishaji kwa kadiri ya uwezo wake
kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha sambamba na kuendelea na
kazi mablimbali kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu.
“NEC
inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kuanza kwa awamu ya pili ya
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mikoa ya Iringa,
Lindi, Ruvuma na Mtwara ambalo litaanza 24 Aprili mwaka huu.
“Tume
tayari imepokea BVR Kits 248 ambazo zinahitajika kufika mapema
kuendeleza mafunzo, lakini leo tume inapokea BVR Kits 1,600 zinazokuja
kwa ndege ya kukodiwa,” amesema.
Jaji
Lubuva ameongeza kuwa, BVR Kits hizo zitatumika katika mikoa
wanayoelekea kuandikisha na ifikapo 24 Aprili, wanategemea kupokea BVR
Kits zingine 1,600.
Amesema
“BVR Kits hizo zitawezesha kuandikisha katika mikoa ya Dodoma, Mbeya,
Katavi na Ruvuma. Uandikishaji katika mikoa hiyo utaanza 2 Mei mwaka
huu. Halikadhalika zitafuata BVR Kits 1,152 ambazo zitawezesha tume
kufanya uandikishaji katika mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma na Kagera
katika tarehe itakayopanga baadaye.”
Kwa
mujibu wa mwenyekiti huyo, BVR Kits hizo zitagawanywa katika
halmashauri ambapo itawezesha wapiga kura wote kuandikishwa ndani ya
siku 28 kila halmashauri.
Hadi
sasa Serikali imetoa dola za Kimarekani milioni 72 (Sh. bilioni 133).
Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya NEC kupokea mashine 2,098, huku
ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa.
Vifaa hivyo vinanunuliwa
na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo
imeingia mkataba na NEC na inaviagiza kutoka China.
Post a Comment