JENERALI BUHARI NDIYE RAIS MPYA WA NIGERIA
Kiongozi wa wa chama cha upinzani
cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na
kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan mamlakani.
Tayari rais
anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha mpigia simu mpinzani
wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo .
Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.
CHANZO: BBC SWAHILI
Post a Comment