KHA! HEMED ASAKWA NA POLISI KWA UTAPELI WA NGUO ZA SH 700,000
Kha! RB namba KTN|RB/11213/2014 –UTAPELI inamsaka msanii wa muziki na
sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ tangu mwaka jana, akidaiwa
‘kuchikichia’ nguo za shilingi laki saba, mali ya aliyekuwa Mtangazaji
wa EATV, Nasra Dattani ‘Lady Naa’ ambaye alimkabidhi begi lake la nguo
baada ya kumaliza kurekodi filamu iitwayo Catherine.
“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.
Alidai kwamba baada ya kumzungusha kwa muda mrefu ndipo alipoamua kumfungulia kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar ambapo hadi leo anasakwa. Baada ya habari hizo kulifikia gazeti hili, mwanahabari wetu alimwendea hewani Hemed lakini namba yake haikupatikana hivyo jitihada zinaendelea.
Msanii wa muziki na sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lady Naa alisema kuwa alimvumilia
Hemed kwa muda mrefu kwani alimpa mzigo huo na kumuomba akaushushe
dukani kwa rafiki yake maeneo ya Kinondoni lakini hakufanya hivyo na
alipokuwa akimkumbusha alikuwa akimwambia kuwa atampelekea.“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.

Post a Comment