AMTOROKA BWANA’KE AJIACHIA NA MIDUME MITANO
BINTI
aliyefahamika kwa jina moja la Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu,
hivi karibuni alimtoroka bwana’ke na kuonekana akijiachia hovyo na
wanaume watano tofauti katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini
Dar es Salaam kulipokuwa na onyesho la Bendi ya Taarabu ya Mashauzi
Classic.
Akionekana kuwa ‘vizuri’ kichwani, kwa kiburudisho alichopata usiku mnene, binti huyo alionyesha umahiri mkubwa wa kukata mauno kiasi cha kuwavutia wanaume ambao kila mmoja alitaka kuwa naye karibu kiasi cha kumfanya kuwa bize kwa kila wimbo kulazimika kucheza na wanaume tofauti.
Baadhi ya wanawake waliokuwa na waume zao jukwaani, walionyesha kukasirishwa na mwenzao huyo, kwani licha ya kuwa hodari wa kucheza, pia aliwaruhusu wanaume kumkumbatia kadiri walivyopenda, kiasi cha kusababisha wakware wengi kuwa na hamu ya kushiriki naye.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo walisema mrembo huyo alitia aibu kwani kuna wakati alicheza hadi nguo zake za ndani zikawa zinaonekana.
“Hii ni aibu jamani, mke wa mtu kucheza namna hii mbaya zaidi hadi nguo inamvuka yeye hata habari hana,” alisema mmoja wa mashabiki.Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo hilo, mrembo huyo alikuwa akiendelea kufanya mavituz yake jukwaani.

Post a Comment