AMINI: SIOGOPI KUIBIWA MKE
BAADA ya mke wa msanii wa Bongo Fleva, Amini
Mwinyimkuu, Farida kujitosa kwenye muziki huo, mumewe ameibuka na kusema
kuwa kamwe haogopi kuibiwa na wakware.Akipiga stori na Over The
Weekend, Amini alisema mke wake ni muimbaji mzuri sana na ndiyo sababu
iliyomfanya amshirikishe kwenye wimbo wake mpya anaotarajia kuuachia
hivi karibuni.
Mbali na hayo Amini aliendelea kufunguka kuwa kama kuna msanii atahitaji kufanya kolabo na mkewe basi inabidi amsikilize kwanza na kisha waelewane juu ya hilo bila kusahau kumtangaza kimuziki.
Msanii wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu akiwa na mkewe.
“Nikiweka fikra za kuibiwa mke hatutasonga kimuziki wala kimaisha na
kwa sababu hakuna kitakachokuwa kikiendelea kati yetu, mimi namuamini na
yeye ananiamini vilevile na mambo kama hayo hayatakuwa na nafasi kwetu
kama tukishikamana vizuri,” alisema Amini.Mbali na hayo Amini aliendelea kufunguka kuwa kama kuna msanii atahitaji kufanya kolabo na mkewe basi inabidi amsikilize kwanza na kisha waelewane juu ya hilo bila kusahau kumtangaza kimuziki.
Post a Comment